KLABU
ya Yanga SC imeipa siku tano Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es
Salaam kutoa idhini ya kujenga Uwanja wa kisasa katika eneo la Jangwani
mjini hapa, vinginevyo wataandamana kushinikiza suala hilo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya
Jangwani na Twiga mjini hapa mchana wa leo, Katibu wa Baraza la Wazee la
Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema wamebaini wanawekewa vikwazo na
baadhi ya madiwani wa Manispaa hiyo.
Mishipa ya shingo; Mzee Akilimali katikati akizungumza na Waandishi wa Habari ,leo Jangwani |
“Jana
kulikuwa na kikao cha baraza la madiwani na Yanga tuliomba tuhudhurie
kikao hicho kwa sababu moja ya ajenda ilikuwa ombi letu la kuongezwa
eneo na kibali cha ujenzi wa Jangwani City. Cha kusshangaza tulikatazwa
kuingia kwenye kikao hicho na kukalishwa nje ya ukumbi kwa saa 10,”
amesema Akilimali ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa ameagizwa na uongozi
wa Yanga azungumze na waandishi baada ya kuzuiwa katika mkutano mkuu
uliopita wa wanachama wa klabu hiyo.
credit: Bin Zubeiry
Post a Comment