Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZIFAHAMU SABABU ZA RIDHIWANI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE ... AWAPASHA WAGOMBEA WENZA

ridhiwaniMGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amewataka wakazi wa Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombea wa Chadema kuwa yeye si mkazi wa Chalinze.


Ridhwani alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejesha fomu za kugombea Ubunge wa jimbo hilo. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chadema, Matayo Torongey, alinukuliwa akisema kuwa Ridhwani hawezi kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa si mkazi wa jimbo hilo.

 
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Ridhwani alionesha kushangazwa kuwa iweje akashifiwe kuwa yeye si mkazi wa Chalinze.

“Yani (Torongey) anaweza kuniambia kuwa mimi sio mkazi wa Chalinze? Hii inachekesha sana kwa kuwa kwanza ni nani asiyejua kuwa mimi mzaliwa kabisa wa huku?” Alihoji Ridhwani.


Aliongeza kuwa ili kuwahakikishia wakazi wa Chalinze maendeleo, wagombea wanatakiwa kutangaza sera zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia ya kuwapumbaza wakazi wa Chalinze.



Alisema kuwa hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza kulumbana na kukejeli, kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya kisiasa.


Alisema hajatokea chumbani kugombania Ubunge, badala yake amekuwa katika misingi ya kisiasa tangu mdogo na amechukua uamuzi wa kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia wananchi.

“Najua awali wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa kuna ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji nayo yanaongezeka,” alisema Ridhwani.

Aliongeza kuwa ongezeko hilo limesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya huduma mbalimbali kama hizo za kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua kero hizo.


“Watu wanadhania kuwa mimi nimetokea chumbani kuja kwenye siasa… hapana yaani tena hata sio kwa sababu ya kuwa mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura huku, sio ila ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni wakati wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa huku,” alisema Ridhiwani.


Kuhusu tatizo la migogoro katika jimbo hilo, alisema anaona kuwa analo jukumu kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM kwa muda mrefu imekuwa ikifanya hivyo.


Alisema atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu ya wafugaji na wakulima.

Ridhwani anatarajia kuzindua rasmi kampeni zake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze lililoachwa wazi kutokana na kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Said Bwamdogo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top