Mwanamume
mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde
la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu
kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa
mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea
Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa
Rift Valley
Mwanamume
huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa
kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.
Mwanamume
huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu
kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji
katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo
alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa
wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba
huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka
katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka
watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili
kuzuia mikosi.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment