Mwanamama
ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca
Kilwai mwenye namba WP 5367 anayedaiwa kuiba mtoto wa jinsia ya kiume
aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7).
SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 na picha yake kudaiwa ‘kuminyiwa’ na askari wenzake ili isionekane, hatimaye Ijumaa Wikienda limeinasa.
Ilielezwa kuwa, mtuhumiwa alishirikiana na
baba mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa
Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi (Mboka Mwakikagile umri
miaka 20) kuwa Prisca ni shangazi yake hivyo amekwenda kumwona mtoto
aliyezaliwa ndipo akatoroka naye.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 17, mwaka
huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na
mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa Makao Makuu ya
Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku hiyo mama
huyo alikuwa katika harakati za kutokomea kusikojulikana lakini bahati
nzuri polisi waliimarisha ulinzi.
“Alikuwa ndiyo yupo katika mikakati ya
kutoroka na haikujulikana alikuwa anataka kwenda wapi maana tayari
alishajua kuwa anatafutwa hivyo kutapatapa na kuingia kirahisi katika
mkono wa sheria,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuhojiwa na polisi kujiridhisha
na tuhuma hizo za wizi, mstakiwa huyo alipandishwa katika mahakama ya…na
kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Baada ya kusomewa mashtaka siku hiyo, kesi
iliahirishwa hadi Mei 6, mwaka huu ambapo mshtakiwa aliruhusiwa kupata
dhamana lakini akashindwa kutimiza masharti (wadhamini wawili na hati)
hivyo kurudishwa sero hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kabla ya
kunaswa katika tukio hilo, askari huyo anayedaiwa kuwa ni mama wa
watoto, aliolewa na kuachika miaka kadhaa iliyopita.
Post a Comment