MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Nkasi imemtia hatiani mkazi wa
kijiji cha Kabwe Camp mwambao mwa Ziwa Tanganyika, Halid Mussa (38) kwa
kosa la kumjeruhi mkewe, Mwajuma Idd(23) kwa kumchanja viganja vyake na
kifuani kwa kisu kwa kile kilichodaiwa wivu wa kimapenzi.
Mshtakiwa huyo ambaye alihukumiwa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Ramadhan Rugemalira ameanza kutumikia kifungo cha miezi sita baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh 100,000.
Mshtakiwa huyo ambaye alihukumiwa jana na Hakimu wa Mahakama hiyo, Ramadhan Rugemalira ameanza kutumikia kifungo cha miezi sita baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh 100,000.
Akitoa hukumu hiyo, Rugemalira alidai mahakamani hapo kuwa upande wa
mashtaka ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi,
Hamimu Gwelo umeithibitishia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa kweli alitenda
kosa hilo. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo
Desemba 27, mwaka jana usiku wa manane nyumbani kwake Kabwe Camp.
Ilidaiwa mahakamani hapo usiku huo wa tukio mshtakiwa akiwa na rafiki
yake aitwae Mhaya walikuwa wakinywa pombe ya kienyeji katika klabu moja
iliyokuwa ikiuza kilevi hicho kijijini humo ambapo rafiki yake huyo
alimuaga akidai kuwa ametosheka kunywa pombe.
Kwa mujibu wa Hakimu, Rugemalira mshtakiwa naye aliamua kurejea
nyumbani kwake na alipoingia ndani alipishana na rafiki yake huyo
akitoka chumbani alimolala mkewe.
Akijitetea mahakamani hapo mshtakiwa aliiomba mahakama hiyo
impunguzie adhabu kwa kuwa anatunza watoto watano alioachiwa na marehemu
mkewe wa kwanza.
Hata hivyo Mwendesha Mashitaka, Gwelo aliiomba mahakama hiyo itoe
adhabu kali kwa mashtakiwa ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia
ya kunyanyasa wanawake ambapo sasa tabia hiyo imekuwa tatizo.
NA PETI SIYAME
Post a Comment