Wakati
watu wengine wanakesha kutafuta watoto lakini pia wadau mbalimbali
wakiendelea kupiga vita ukatili dhidi ya watoto,vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto vimeendelea kujitokeza katika jamii ambapo huko katika
kijiji cha Senane wilayani Maswa mkoa mpya wa Simiyu mwanamme mmjoa
aitwaye Baya Seni amekuwa akimpa mateso makali mtoto wake wa kiume
mwenye umri wa miaka minne ili afe kwa madai kuwa hapendi watoto wa
kiume.
Baya
Seni ambaye ni mkazi wa kijiji hicho cha Senane amekuwa akimpa mateso
makali mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Amos Baya mwenye umri wa
miaka minne toka kuzaliwa kwake hali iliyoelezwa kusababisha mtoto huyo
kudhoofika mwili na kupata ugonjwa wa utapiamlo.
Miongoni
mwa mateso aliyoyapata mtoto huyo ni pamoja na kuvunjwa vidole vya
mkono wa kushoto, kutelekezwa shambani siku zaidi ya mbili bila kula na
kuning'inizwa juu ya mti.
Imeelezwa
kuwa Mwanamme huyo hapendi watoto wa kiume kwa madai kuwa wanaleta
umaskini kwa sababu wakikua watataka kuoa na kuchukua mali, lakini mtoto
wa kike akikua ataolewa na kuleta mali nyumbani.
Taarifa za mtoto huyo kupata mateso kutoka kwa baba yake mzazi zilitolewa na msamaria mwema siku ya tarehe 31 mwezi Machi mwaka huu ambaye
alikwenda katika shughuli za mazishi katika kijiji hicho na kumwona
mtoto huyo ndipo akapiga simu ofisi ya ustawi wa jamii wilaya ya Maswa
na kufuatia taarifa hizo ofisi hiyo iliwataarifu polisi na wakaenda
kumchukua mtoto huyo na kumuweka chini ya ulinzi baba mzazi wa mtoto
huyo.
Afisa ustawi wa jamii wilayani maswa Bwana Husein Mshana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Hivi sasa mtoto huyo amelazwa wodi namba nane ya watoto katika hospitali ya wilaya ya Maswa akipatiwa matibabu.
Mama mzazi wa mtoto huyo Elizabeth Paul amekiri kuwa mtoto huyo amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili na baba yake mzazi na kwamba hata yeye amekuwa akipewa vitisho kuwa endapo atasema atauawa.
Tayari baba mzazi wa mtoto huyo Amos Baya anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani maswa kwa hatua za kisheria.
Na Veronica Natalis-Simiyu
|
Post a Comment