Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dkt. Kigoda: Fanyeni kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu mkubwa

 


???????????????????????????????
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda( Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Uledi Mussa( Kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Maria Bilia (Kulia), wakifuatilia mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika JijiniDsm.
???????????????????????????????
Waziri wa Viwanda na Biashara DktAbdallah Kigoda akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake unaofanyika JijiniDsm.
???????????????????????????????
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizaraya Viwanda na Biashara ambao ni wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wanaoshiriki mkutano wao JijiniDsm
…………………………………………………………………………..
Wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wametakiwa kuongeza juhudi na ubunifu katika utendaji wa kazi ili kuiwezesha Wizara hiyo kufikia malengo yake iliyojiwekea.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.DktAbdallah Kigoda, wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa siku mbili Jijini Dar Es Salaam.
Dkt. Kigoda amesema, Wizara ya Viwanda na Biashara ina jukumu kubwa katika kuboresha Uchumi wa Nchi hivyo wafanyakazi hawana budi kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuiwezesha Wizara kupata matokeo yaliyokusudiwa.
“Fanyeni kazi kwa bidii, kwa maarifa na ubunifu mkubwa. Epukeni uzembe, ukiritimba usio na sababu za msingi na zaidi ya yote, tujitangaze ili Umma ufahamu kikamilifu jitihada zetu katika kukuza uchumi’’.
Awali akimkaribisha Mh Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Uledi Mussa amesema, Uongozi wa Wizara hiyo utaendelea kufanya jitihada za kuboresha maslahi ya wafanyakazi, mazingira ya kufanyia kazi na kuondoa kero mbalimbali zinazowakwaza watumishi.
Kwa upande wake Mtoa mada katika Mkutano huo Bi Honesta Ngolly ambae ni Afisa Elimu Kazi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, amewataka watumishi na Viongozi wa Wizara kutimiza wajibu wao, kuheshimu sheria na miongozo ya kazi ili kuepusha migogoro katika sehemu za kazi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top