MWASISI na muandaji wa Miss Tanzania, Hashimu
Lundenga, ‘Uncle Lundenga,’ amefunguka kuwa wanaoshinda Umiss Tanzania
hawashindi kwa rushwa ya ngono.
Lundenga (58) Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni
waandaaji wa mashindano ya urembo Tanzania ni mmoja wa wadau muhimu sana
katika tasnia ya urembo, alianza kujihusisha na kuendesha mashindano
hayo ya Miss Tanzania mwaka 1994 ambapo ndipo shindano la kwanza
lilifanyika nchini.
Akizungumza katika chumba cha habari cha Global Publishers maeneo ya
Bamaga, Mwenge, jijini Dar, Lundenga alisema mashindano hayo hayampi
ushindi mrembo kwa sababu ya kutoa rushwa ya ngono ama pesa kama wengi
wanavyodhani bali mshindi hupatikana kutokana na uwezo wake wa kukidhi
vigezo.
Mwandishi: Mashindano ya urembo uoni kama yanakuwa kinyume na utamaduni wa Mtanzania kwa wasichana kuonyesha maungo yao?
Lundenga:
Mwaka 1995 ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa wasichana kupita
jukwaani na beach wear (vazi la ufukweni) ingawa wasichana na Watanzania
wenyewe ndiyo walitaka kupita hivyo. Hata hivyo, sioni kama ni sahihi
mbona watu wa kijijini wanaoga mitoni na wanaume wanapita na wanaona
chuchu za wanawake, kwa hiyo nao wanakiuka utamaduni?
Mwandishi:
Ulishawahi kupokea rushwa ya pesa ama ngono ili kumpa mrembo ushindi?
Hashimu: Haijawahi kutokea na ninaheshimu mashindano haya kama kazi
yangu na isitoshe mimi nina mke na familia yangu.
Mwandishi: Unazungumziaje skendo za kuwauza warembo kwa mapedeshee? Lundenga:
Binafsi siwezi kufanya ujinga huo, baadhi ya mapedeshee (watu
wanaomwaga fedha kwa warembo na wasanii jukwaani) nawafahamu lakini
sijawahi kujaribu kitu kama hicho na siwezi kumpa mtu ushindi kwa
kumuuza au kumtumia, tulishawahi kumpa
onyo na kumsimamisha mwanakamati mmoja kwa utovu wa nidhamu na ujinga wake.
onyo na kumsimamisha mwanakamati mmoja kwa utovu wa nidhamu na ujinga wake.
Mwandishi: Kufuatia muda mwingi kuwa na warembo, unapata vikwazo vipi kutoka kwa mkeo?
Lundenga: Hakuna vikwazo kwa sababu hata yeye alikuwa mmoja wa washiriki mwaka 99 na nilimuoa baada ya mashindano siyo ndani ya mashindano.
Mwandishi: Ulishawahi kutegwa na msichana katika uandaaji wa mashindano ili umpe ushindi?
Lundenga: Hayo mambo yapo tena sana, wapo baadhi ya wasichana wanaokuja katika mashindano wakiwa tayari kwa kila kitu ili washinde na wasichana kama hawa wanapita sana na kujilegeza kwa wana kamati.
Mwandishi: Mashindano yanaonekana kama yamepunguza mvuto, ni kweli?
Lundenga: Ni kweli hata sisi tumegundua hilo lakini ukumbuke mashindano haya yana miaka 20 sasa hapa nchini, ni muda mrefu.
Inawezekana yamepungua mvuto kwa sababu yame zoeleka sana labda
hayana kipya, tatizo ni kwamba hatuwezi kubadilisha muundo wa mashindano
kwa kuwa hata waandaaji wa Miss World (mrembo wa dunia),
hawajabadilisha taratibu.
Kama tukibadilisha tukawekavionjo vyetu haitakuwa Miss Tanzania tena.
Mashindano kwa ngazi ya taifa hayajapungua mvuto labda kwenye matangazo
ndiyo yamepungua.
Aidha, Lundenga alisema pamoja na changamoto nyingi zinazowakabili
ikiwemo ya kukosa mdhamini mkubwa wa uhakika, wazazi kufikiri kuwa
mashindano hayo ni uhuni n.k, lakini Watanzania wana kila sababu ya
kulithamini shindano hili kwani kufika Miss World ni jambo la kujivunia
sana.
“Tanzania kufika Miss World ni sehemu kubwa sana ya kujipongeza
kwani nchi zinazoshiriki ni zaidi ya 120 na Tanzania tulifanikiwa kufika
nafasi ya sita, ni jambo la kujivunia sana,” alisema.
CHANZO: GPL
Post a Comment