Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kapombe rasmi Azam, apewa jezi namba 33



http://www.mwanaspoti.co.tz/image/view/-/2082754/highRes/627536/-/maxw/600/-/12qr8gq/-/kapombe.jpg KIUNGO kiraka Shomari Kapombe, sasa mambo safi na amekamilisha kila kitu kurejea kucheza soka nchini na tayari amemalizana na klabu ya Azam FC na amekabidhiwa jezi yake kabisa.
Imefahamika kuwa Kapombe amekubali kujiunga na Azam kutokana na kutokuwa katika maelewano mazuri na AS Cannes aliyojiunga nayo akitokea Simba, mwaka jana. Habari za uhakika, asilimia mia, Kapombe ameishavunja mkataba na Wafaransa hao, ndiyo maana amekubali kujiunga na Azam FC ambayo imekuwa ikifanya naye mazungumzo kwa zaidi ya mwezi sasa. Taarifa za uhakika kuhusu Azam na Kapombe ambazo zimetua kwenye meza ya Championi Jumatatu zinaeleza kuwa, usajili huo umekamilika kila kitu kwa dola 100,000 (Sh milioni 160) kisha Kapombe kupewa jezi namba 33, ambayo ataitumia msimu ujao, huku akiwa ameanza mazoezi kwenye Uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na timu hiyo. “Tayari Azam wameshamsajili Kapombe, ameshapewa na ratiba ya mazoezi kwenye Uwanja wa Chamazi. Azam walishawasiliana na uongozi wa AS Cannes ambao nao umeridhia baada ya kupewa walichokihitaji, kwa hiyo Kapombe na AS Cannes basi tena, sasa hivi ni Azam,” alisema mtoa taarifa wetu. Kapombe alisajiliwa bure na AS Cannes lakini alirejea nchini kuitumikia Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe kisha hakurudi tena Ufaransa na tangu hapo kumekuwepo na danadana nyingi kuhusu usajili wake.
Akizungumzia juu ya taarifa hizo, mtu kutoka ndani ya AS Cannes aliliambia Championi Jumatatu: “Kapombe ameshavunja mkataba na sisi, lakini bado kuna kesi yake ipo Fifa, tunasubiri majibu kwanza, halafu tutalizungumzia.”
Alipopigiwa simu wakala wa mchezaji huyo, Denis Kadito anayeishi nchini Uholanzi, hakupatikana wakati Azam nao walikuwa bize na mechi dhidi ya Simba, hivyo hakukuwa na kiongozi aliyepatikana.
Gazeti hili lilimtafuta Kapombe kuhusiana na suala hilo naye alifafanya kwa ufupi.

“Habari za kusaini Azam sasa bado mimi ndiyo nimeomba kufanya mazoezi kwa kuwa napata vifaa vyote pale.
“Najua mambo yanasemwa mengi, lakini sasa si muda mwafaka. Ila naendelea na mazoezi ili kama ikitokea timu inanihitaji, basi niwe fiti,” alisema Kapombe akionyesha kujiamini.

Lakini mmoja wa maofisa kutoka ndani ya Azam FC alisisitiza kuwa Kapombe amemalizana na Azam na suala la mshahara limepitishwa.
Kapombe alipelekwa bure AS Cannes, Simba ilikuwa inategemea kupata asilimia 40 ya mauzo yake, lakini sasa imeangukia pua.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibhxtHNtM_AwUxSAE-R-JDL-wtpWdPPjME2IC9xOyUUPYVKaMvj-2woHyqz3bobKgeDlP-Wxuqdka2NGuaCJRpAmns2r4915SBjxXcKY85bxM1B9dg95-MjpnxooOIOimjEGRVAvmI7doX/s640/kapombe.tiff 
Ukiachana na As Cannes, Fc Twente inayoshiriki Ligi kuu ya Uholanzi ambayo ni moja ya Ligi kubwa barani ulaya iliypwatoa nyota kama Van Persie,Wesley Sneijder na wengine wengi nayo ilikuwa na mchakato ya kuhakikisha inamtwaa kiungo huyo kiraka wa Simba kabla ya kutua Fc Cannes


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top