Zikiwa
zimepita takribani siku nne tangu Azam FC ilipoandika historia ya
bingwa wa mpya wa ligi kuu ya Vodacom huku tetesi zikizidi kuzunguka
mitaani kwamba klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam imekuwa ikihonga sana
wachezaji wa timu nyingine pamoja na marefa ili kujihakikishia ushindi
na hatimaye kutwaa ubingwa kabisa.
“Maneno yanayozungumzwa ni porojo Baada ya Azam Fc kupata
mafanikio ya kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam Fc ilipata
nafasi ya pili mara Mbili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara haikuwai
kusemwa imenunua leo iweje imekuwa Bingwa isemwe imenunua.John Bocco ameweka Historia Baada ya Kufunga Goli la Ushindi ktk Mechi ya Mwisho ya Ligi Daraja la kwanza na Kuipandisha Azam Fc kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara, na leo Hii Tumeshuhudia John Bocco ameweka Historia ya Kufunga Goli la Ushindi na Kuipa Timu ya Azam Fc Ubingwa kwa Mara ya kwanza Tangu ilipopanda Daraja kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu 2013/2014 na kucheza Bila kupoteza hata mechi Moja.
Hatuto puuzia mechi ya mwisho Dhidi ya JKT Ruvu Tutacheza
kama mechi nyingine Tulivyocheza Tunahitaji kuweka Historia ya
Kutokupoteza hata Mechi Moja kwa Msimu Huu JKT Ruvu wajiandae kwa
Kichapo wakati Tukiwa Tunakabidhiwa Kombe letu la Msimu Huu
Baadhi ya Maneno ambayo Makocha wanazungumza Sio Mazuri wao kama wataalam hawatakiwi kujihusisha katika Propaganda ambazo baadhi ya watu wanaziendeleza.”
Baadhi ya Maneno ambayo Makocha wanazungumza Sio Mazuri wao kama wataalam hawatakiwi kujihusisha katika Propaganda ambazo baadhi ya watu wanaziendeleza.”
Post a Comment