- Asisitiza Umoja na Mshikamano Kigoma
- Asema ahadi zote zitatekelezwa
- Awataka Viongozi wa CCM kufanya mikutano mingi na wanachama na wananchi kwa jumla
- Nape afundisha Umma Demokrasia ya kweli,aonyesha namna gani vyama vingi vya upinzani ni wababaishaji atolea mifano namba alivyotelekezwa mgombea wa Chalinze
- Zaidi ya wanachama 350 wajiunga na CCM
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya
Kigoma mjini bila kujali mvua,ambapo alisisitiza kuwa CCM itatekeleza
kila walichoahidi.
Viti
vikitumika kujikinga na mvua iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano wa
CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre wilaya ya
Kigoma mjini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye (wa kwanza kulia),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Dk. Aman
Walid Kaborou, Balozi Karume na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu
Issa Machibya wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu wakati wa mkutano wa
hadhara bila kujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Mbunge
wa Kigoma mjini Mheshimiwa Peter Serukamba akiwahutubia wakazi wa
Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Mwanga Community Centre na kuwaambia kuwa Kigoma imebadilika na bado
anapigania wananchi hao wapate maji salama na ya kutosha.
Upinde
wa Mvua unaonekanika kabla mvua kubwa haijanyesha kwenye viwanja vya
Mwanga Community Centre ambapo mkutano mkubwa wa CCM ulikuwa unafanyika.
:
Mjumbe
wa NEC Balozi Ali Abeid Karume akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini na
kuwaambia kuwa Muungano wa Serikali mbili ndio Muungano pekee
utakaodumisha Umoja miongoni mwa wananchi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa
Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Mwanga Community Centre ambapo aliwaambia kuwa vyama vya upinzani
vinaelekea kutoweka mapema kabla hata havijakomaa kidemokrasia.
Post a Comment