JESHI la
Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Songambele
wilayani Maswa mkoani hapa, kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto wake kwa
kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba ili aliwe na fisi.
Kamanda
wa polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo alisema ofisini kwake mjini hapa
jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane za usiku wakati
mtuhumiwa Baya Seni (30) akiwa amelala na familia yake kijijini hapo,
ndipo alipokurupuka ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na kisha
kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba.
Alisema,
Seni katika maelezo yake kituo cha polisi alisema alifikia uamuzi huo
kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani
uzoefu umeonesha kuwa watoto wa kiume wakikua hudai kupata mirathi
kutoka kwa wazazi wao .
Alisema kinyume chake watoto wa jinsia
ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa mifugo atakapolipwa mahari ili
waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigo tena kwenye familia yake bali
mzigo huo huhamia kwenye familia atakayoolewa. Mtoto huyo aliokolewa na
majirani baada ya kusikia kilio.
Mama wa
mtoto huyo Elizabeth Paulo alisema, mume wake alikuwa akimtesa sana
mtoto wake akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na kwamba hana
faida kwa
Post a Comment