Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe,
sehemu ya Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam,
lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini,
wakati Makamu alipofanya ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa
daraja hilo leo Aprili 13, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wanaosimamia shughuli ya daraja
hilo, baada ya kuwasili eneo hilo leo.
Sehemu
ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika
kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza
kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia
hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja.Picha na OMR
Post a Comment