Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Matukio ya picha za wajumbe bunge maalum la katiba Kamati mbalimbali leo mjini Dodoma

 

       zendi
kmt 10 mjadala
hamadMwenyekiti wa Kamati namba tano(5) ya Bunge Maalum la Katiba Hamad Rashid Mohamed (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
kilanggMwenyekiti wa Kamati namba kumi na moja(11) Anna Kilango akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati wanapitia rasimu ya Katiba mpya. kimiitMwenyekiti wa Kamati namba kumi(10) ya Bunge Maalum la Katiba Paul Kimiti (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya. kmt 4 a
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Salehe Nassoro Juma akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya. kmt 10 mjadala
Baadhi ya wajumbe wa  Bunge Maalum la Katiba ,Kamati namba nne (4) wakiwa katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
kmt nne
Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba Dr. Sira Ubwa Maboya (kushoto) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya. lowasa
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) akijadiliana na Mjumbe mwenzake Selemani Jafo leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya makind
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(kulia)  akitoa mchango wake leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati namba mbili(2) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
  salehe
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Machano Othman Said  akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
selathini
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Joseph Selethin akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba tano (5) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya. waandishiMwenyekiti wa Kamati namba tano (5) Hamad Rashid Mohamed akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati wanapitia rasimu ya Katiba mpya. wajumb
Baadhi ya wajumbe wa  Bunge Maalum la Katiba , Kamati namba tano (5)wakiwa katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
wajumbe na Lowasa
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kulia) akisamiliana na wajumbe wenzake leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
zendi
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Zendi Mvano Abdallah  akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba kumi (10) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.

**********
Na        Magreth Kinabo – Dodoma
 Kamati 12 za Bunge Maalum  zimeaanza kazi vizuri ya  kuchambua Rasimu ya Katiba, huku baadhi ya wenyeviti wakisema kuwa muda wa siku mbili wa kujadili sura ya kwanza na ya sita  hautoshi.
 Hayo yamebainika  katika mahojiano  ya Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya Bunge hilo, Anne Kilango Malecela, yayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper  mjini Dodoma.
“ Tatizo lililojitokeza ni kwamba muda wa siku mbili hautoshelezi , leo tumejadili  sura ya kwanza sehemu ya kwanza kesho tutajadili sehemu ya  pili ya sura ya kwanza hivyo tunaweza tusiiguse sura ya sita.
“ Wenzetu walikakataa Kanuni zisirekebishwe. Lakini  wenzetu wapinzani wameliona hilo wameanza kusema muda hautoshi,” alisema  Anna .
 Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo atamweleza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitaa (leo jioni ) kuwa  muda hautoshi.
 Mwenyekiti huyo  tatizo lingine lililojitokeza katika  kamati yake ni baadhi ya wajumbe kutokuwa na uelewa wa tofauti ya dola na nchi, hali iliyomfanya kutumia kanuni namba 56(7) kumwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo  ikiwezekana  kumleta  mtaalamu wa sheria ili kuweza kutoa elimu hiyo  leo (jioni) juu ya masula hayo.
 Akizungumzia kuhusu mjadala alisema wajumbe wote walijitayarisha vizuri na walishindana kwa hoja hivyo hakuna aliyetoa maneneo makali.
Akizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo, kwa sababu alikuwa katika  Mwenyekiti wa  Kamati namba moja ,Ummy Ali Mwalimu alisema  wajumbe walichangia kwa   utulivu.
 Ummy  alisema kilichojitokeza katika kamati yake ni kuwa muda hautoshi  kama ilivyodaiwa na baadhiya wajumbe kutoka upinzani, chama tawala na kutoka 201.
Naye  Mwenyekiti wa Kamati  ya  namba tano ya Bunge hilo ,Hamad Rashid  alisema kamati yake mjadala unaendelea vizuri na ulikuwa wa kistaarabu.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top