Mwanadada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kwa sasa yupo tayari kuigiza nusu uchi kwa sinema za nje ya nchi.
Akiongea nasi juzi kati, Batuli alisema kuwa muvi nyingi Bongo huwa zinafungiwa kwa kukosa maadili na kwamba kama ikitokea nafasi akaitwa nje ya nchi kuigiza sini hizo, atakuwa tayari.
“Zamani nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu uchi. Wenzetu Nigeria wameendelea na ndiyo maana wanaigiza hata nusu uchi, kama itatokea nafasi ya kuigiza huko (nje ya Bongo) nusu uchi, nipo tayari,” alisema Batuli.
Post a Comment