Mkurugenzi
wa Utawala na Masoko kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Stanley
Mahembe akiwatambulisha wageni walioketi meza kuu (hawapo pichani)
wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini,
mafunzo hayo yamefungwa jana Mkoani Morogoro.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwahutubia
Wasimamizi na Wadadisi (hawapo pichani) muda mchache kabla ya kufunga
mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini, mafunzo hayo
yamefungwa jana Mkoani Morogoro.
Baadhi
ya Wasimamizi na Wadadisi wa Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini
wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel
Bendera (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi hilo jana
Mkoani Morogoro.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na maofisa wa Serikali pamoja na Wasimamizi wa
Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini mara baada ya kufunga mafunzo ya
zoezi hilo jana Mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
…………………………………………………………………………………
Na Veronica Kazimoto, Morogoro
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera ametoa wito kwa Wamiliki wa
viwanda nchini kutoa ushirikiano kwa Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la
Uorodheshaji wa Viwanda kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda
inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.
Akiwahutubia
Wasimamizi na Wadadisi wakati wa kufunga mafunzo ya zoezi hilo mkoani
Morogoro, Bendera amesema ni muhimu kwa Wamiliki wa viwanda kutoa
ushirikiano kwa wadadisi ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata takwimu
sahihi ya orodha ya viwanda vilivyopo nchini.
“Natoa
wito kwa Wamiliki wote wa viwanda nchini kutoa ushirikiano kwa Wadadisi
kwa kuwapatia takwimu sahihi za viwanda vyao, wakifanya hivyo, zoezi
hili litafanikiwa kwa ufanisi mkubwa sana” amesema Bendera.
Aidha,
Bendera amewatoa wasiwasi Wamiliki wa viwanda kwa kusema kuwa zoezi
hili la Uorodheshaji wa Viwanda halitaathiri shughuli zozote za
viwandani.
Awali,
akitoa maelezo ya utangulizi, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu Bw. Morice Oyuke amesema, baadhi ya taarifa
zitakazokusanywa katika zoezi hilo ni pamoja na anuani za viwanda,
mahali viwanda vilipo, aina ya umiliki na utaifa wa mmiliki.
Taarifa
nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato
yanayotokana na uzalishaji, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa
zinazozalishwa, idadi ya wafanyakazi na gharama za uzalishaji.
Zoezi
la Uorodheshaji wa Viwanda linahusu viwanda vidogo, vya kati na vikubwa
na litafanyika nchi nzima kwa muda wa miezi miwili kuanzia mwezi huu
Aprili mpaka Juni, 2014.
Post a Comment