Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Sentensi 12 za alichosema Juma Duni Haji kwenye bunge la katiba leo.

 

Screen Shot 2014-04-11 at 1.51.39 PM 
akiwasilisha maoni ya wachache kutoka kwenye kamati namba 11 ambapo alianza kwa kusema >>> ‘hoja za wengi ni muundo serikali ya shirikisho kuua udugu, kwani kabla ya muungano hatukua na udugu’
Kuna
wajumbe wanasema kuirudisha serikali ya

Tanganyika ni kufufua makaburi, kwani imezikwa? ninachofahamu mimi Tanganyika imekufa kwa kubadilisha jina tu.
Wengine
eti serikali3 zitarudisha usultani Zanzibar, Loooooh! Mashaaalah, baada
ya miaka 50 tunayazungumza haya? katiba ya sasa kifungu 98b kimetoa
ruhusa Watanganyika na Wazanzibar wakikubaliana muungano utavunjika sio
lazima serikali 3.

Mabunge ya sasa yana wajumbe wasiopungua 438 ya serikali 3 yatakua na 314 sasa mtu anaibuka tu na kusema serikali 3 gharama.
Ikaelezwa
Zanzibar kuruhusiwa kutafuta misaada nje kwa nini mliizuia sasa baada
ya serikali 3 mmerejesha? ikaelezwa pia mafuta kuondolewa ktk orodha ya
mambo ya muungano, ni miaka7 hii lilipitishwa, kisa serikali 3 ndio
mnaliondoa?

Katika
dharau tunayofanyiwa kwa udogo wetu Znz tunaambiwa hatuna uwezo
kuchangia muungano, pato la Mznz na Mtanganyika halina tofauti,
Tanganyika ni kubwa lakini kwa mmojammoja umasikini wetu ni sawasawa

Makusanyo
ya muungano yanayotumika kwa muungano hayajazidi 35% ambapo si chini ya
60% yaliyobaki yanatumika Tanganyika, hizi tume ambazo haziundwi na
account kutofunguliwa ni kwa sababu mapato haya Znz haitakiwi kupata.

Sifa ya Zanzibar kwa miaka 50 kama serikali hizi mbili kweli zilikua na nia njema, Zanzibar ingekua sasa Hongkong ya Afrika.
Znz
haina benki kuu wala sarafu yake na sera zote za uchumi ziko chini ya
Muungano, Zanzibar mmeifunga miguu na mikono, leo kutatua matatizo ya
Muungano kwa mfumo wa serikali 3 linatangulizwa swala la gharama, kwani
lini zilikua ndogo?

Nilisoma
kwenye magazeti miaka 50 uhuru wa Tanganyika si chini ya Bilioni 70
zimetumika katika sherehe, sherehe zenyewe za uwanja wa taifa kutazama
gwaride watu wanavyorusha viatu, hayo hayo miaka yote.

Mikoa
ya Tanganyika wakati wa 64 ilikua 17 tu ila sasa haipungui 26, Wilaya
zilikua 60 mpaka 70 lakini sasa hazipungui 150, kila ukipanua madudu
haya unaongeza gharama za utawala, yanatuhusu nini sisi Wazanzibari
magharama haya?

Alichofanya Warioba ni kujaribu kusahihisha haya ya miaka 50, baada ya kutusaidia wengi mnataka hali hii iendelee?
Hayo ndio yaliyowasilishwa na Juma Duni Haji
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top