Wakazi wa
eneo la Mapinga Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada
ya kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada
ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja
hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika
maeneo mbali mbali hapa nchini.
Akithibitisha kutokea
kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei
amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa
barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara
ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.
Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na
makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza
lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe.
Ukiangalia kati ya hizi picha, kuna moja inaonekana na matete katikati
na pembeni yake, kushoto na kulia yanapita maji. Maeneo haya yanayopita
maji kwa kipindi fulani yalikuwa yakichimbwa mchanga na kuacha katikati
ya mto kuwa na mwinuko. Mvua nyingi maji yamepita pembeni na hata kwenda
nje ya daraja.
Mawasiliano kati ya Dar na Bagamoyo kwa barabara ya Bagamoyo yamekatika.
Maji yanayopita katika mto Mpigi ambako daraja halipitiki ni mengi sana
kiasi kwamba nguzo tatu zinazopitisha umeme mkubwa kwenda Bagamoyo zipo
hatarini. Mojawapo maji yanaikaribia zaidi na uwezekano wa kusombwa ni
mkubwa kwa sababu miti mikubwa iliyokuwa karibu na eneo hilo nayo
imeng'olewa kirahisi kabisa.
on Sunday, April 13, 2014
Post a Comment