Mkuu wa polisi kituo cha pangani anasema gari hilo lilisimamishwa na maafisa wa polisi waliolishuku kwa sababu lilikua likiendeshwa kwenye upande wa kulia wa barabara badala ya kushoto.
Maafisa wawili wa polisi waliingia kwenye Gari hilo na kuliongoza hadi kituo cha polisi cha pangani na baadaye bomu lilokua ndani ya gari hilo kulipuka katika eneo la kuegeshea magari katika kituoni humo na kuwaua watu wanne wakiwemo washukiwa wawili.
Walioshudia wanasema magari mawili yaliokua yakifatana kabla ya lile lilokua mbele kulipuka ndani ya kituo cha polisi cha Pangani ambapo bosco Mugendi mmiliki wa kibanda cha kuuza bidhaa eneo la pangani alinukuliwa na BBC akisema ‘kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje’ CREDITS: TZA
Post a Comment