 |
Pichani ni Mtoto Sabrina Athuman (11)aliyepotea
MWANAFUNZI
aliyefahamika kwa jina la Sabrina Athuman (11) anayesoma darasa la
nne katika shule ya Msingi Kagera iliyopo kata ya Ilomba Jijini Mbeya
ametoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha toka April 26
mwaka huu .
Akizungumza
na Mbeya yetu ,Baba Mlezi wa mtoto huyo, Jumbe Said Zungiza alisema
kuwa mtoto huyo alitoweka nyumbani kwao eneo la Mama John April 26
mwaka huu majira ya saa 1.00 asubuhi bila kuaga.
“Kawaida
huwa tunajua kuwa mtoto wetu siku za jumamosi huwa anaenda shuleni
kwenye mitihani na kabla hajaenda shule kawaida huwa tunampa sh.500 ya
mtihani lakini cha kushangaza siku hiyo tulishtuka kuona hayupo na
kitendo cha kutoaga kilituchanganya ikabidi tuingie chumbani kwake lakin
hatukufanikiwa kumuona mpaka sasa”alisema Baba wa mtoto huyo.
Akizungumzia
kuhusu mazingira ya kupotea kwa mtoto huyo Bw.Zungiza alisema kuwa
mazingira aliyoondoka mtoto huyo yanazidi kuwapa wasiwasi kwani
aliondoka asubuhi sana na kilichowafanya wazazi hao kushtuka ni baada ya
kuamka kuona milango ya nje ipo wazi ndipo walipoanza kuita na
hakuitika.
Aliiongeza
kuwa walimtafuta mtoto huyo mpaka kufika shuleni kwao ambako nako
hakufika kufanya mitihani na ndipo zilipoanza juhudi za kutoa taarifa
polisi,Misikitini lakini hajaweza kupatikana licha ya juhudi zote
kufanyika kwa kushirikiana na ndugu na marafiki .
Kwa
upande wake Mama mlezi wa Mtoto huyo Riziki Jumbe alisema April 26
mwaka siku alipotoweka mtoto huyo nyumbani alivaa SURUALI ya KAKI ,SWETA
yenye rangi mchanganyiko ambayo ni Nyekundu,Kijani ,Bluu,pamoja na
kuvaa Hijabu kichwani Nyeupe.
Aidha
Bi.Jumbe alisema kwamba rangi ya mtoto huyo ni Maji ya kunde ,na mrefu
mwemba mwemba na kwamba mara nyingi anapenda kutembelea maeneo ya
Mswiswi kwa mjomba wake lakini huko hajaweza kufika..
Kwa yeyote mwenye taarifa za mtoto huyo awasiliane na Baba Mlezi wa Mtoto huyo Jumbe Said Zungiza kwa namba 0767810191 au 0715810191,Mama Mlezi Riziki Jumbe 0756684016
|
on Monday, April 28, 2014
Post a Comment