IDARA
ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi , mkoani Kilimanjaro,
inawashikilia wahamiaji haramu 47 raia wa Ethiopia, kwa tuhuma za
kuingia nchini kinyume cha sheria. Mbali na wahamiaji hao, Idara hiyo
inamshikilia Mtanzania mmoja Benjamini Saimon (28) mkazi wa Kibamba, Dar
es salam, kwa tuhuma za kuhusika na kuwasafirisha wahamiaji hao.
Akiongea na FIKRAPEVU Ijumaa, Aprili 4, mwaka huu, Mkuu wa Uhamiaji
mkoa wa Kilimanjaro, Johannes Msumule, alisema wahamiaji hao walikamatwa
Alhamisi ya April 3, mwaka huu, saa 9:30 usiku katika eneo la
Chekereni katika kata ya Kahe Wilaya ya Moshi barabara kuu ya kutoka
Moshi kwendaTanga.
Amesema raia hao wa Ethiopia, walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya
Mitsubish Fuso lenye namna za usajili T216 ASU wakidaiwa kujiandaa
kwenda Afrika Kusini.
“Mwezi wa tano tunaenda katika maeneo ya mipakani kutoa elimu kwa
wananchi wanaoishi kule, kama Kilobo, Kileo, Holili, Kifaru na maeneo
yote ili tuweze kufanya hii kazi kwa kushirikiana na wao” alisema
Msumule.
Hata hivyo, alisema kwa sasa idara hiyo imejipanga vizuri ili kuweza
kutokomeza tatizo la wahamiaji haramu, ambao kwa sasa wameanza
kufuatilia ili kuwabaini watu ambao wamekuwa wakijihusisha na kazi
ya kuwasafirisha. Alisema katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu,
jumla ya wahamiaji haramu 216 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali
nchini.
Alisema jumla ya Kesi 12 zimefikishwa mahakamani ambapo kesi moja imemalizika na nyingine 11 bado zinaendelea.
- See more at: http://www.fikrapevu.com/wahamiaji-47-toka-ethiopia-watiwa-mbaroni-kilimanjaro/#sthash.6GKgFTpC.dpuf
IDARA
ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, mkoani Kilimanjaro,
inawashikilia wahamiaji haramu 47 raia wa Ethiopia, kwa tuhuma za
kuingia nchini kinyume cha sheria. Mbali na wahamiaji hao, Idara hiyo
inamshikilia Mtanzania mmoja Benjamini Saimon (28) mkazi wa Kibamba, Dar
es salam, kwa tuhuma za kuhusika na kuwasafirisha wahamiaji hao.
Akiongea,
Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro, Johannes Msumule, alisema
wahamiaji hao walikamatwa Alhamisi ya April 3, mwaka huu, saa 9:30
usiku katika eneo la Chekereni katika kata ya Kahe Wilaya ya Moshi
barabara kuu ya kutoka Moshi kwendaTanga.
Amesema
raia hao wa Ethiopia, walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya Mitsubish
Fuso lenye namna za usajili T216 ASU wakidaiwa kujiandaa kwenda Afrika
Kusini.
“Mwezi
wa tano tunaenda katika maeneo ya mipakani kutoa elimu kwa wananchi
wanaoishi kule, kama Kilobo, Kileo, Holili, Kifaru na maeneo yote ili
tuweze kufanya hii kazi kwa kushirikiana na wao” alisema Msumule.
Hata
hivyo, alisema kwa sasa idara hiyo imejipanga vizuri ili kuweza
kutokomeza tatizo la wahamiaji haramu, ambao kwa sasa wameanza
kufuatilia ili kuwabaini watu ambao wamekuwa wakijihusisha na kazi ya
kuwasafirisha.
Alisema
katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu, jumla ya wahamiaji haramu
216 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema jumla ya Kesi 12 zimefikishwa mahakamani ambapo kesi moja imemalizika na nyingine 11 bado zinaendelea.
>>fikrapevu
Post a Comment