Waziri
mkuu Mizengo Pinda na mkewe wakitoa heshima za mwisho walipokuwa
wakiuaga mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central
Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo kabla ya ibada ya mazishi iliyofanyika
katika kanisa la roho mtakatifu Dodoma.

Mjane wa
Marehemu aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglican Central Tanganika
Godfey Mhogolo, Iren Mhogolo akiwa mwenye huzuni pembeni ya jeneza
kabla ya kuingizwa kaburini.

Maaskofu
mbalimbali wa kanisa la Aglican wakilishusha jeneza lenye mwili wa
aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Central Tanganika Godfrey Mdimi
Mhogolo kaburini, katika mazishi yaliyofanyika nje ya kanisa la Roho
Mtakatifu maarufu la Mtungi Mjini Dodoma.

Maaskofu
mbalimbali wa kanisa la Aglican wakiweka mchanga kwenye kaburi la
aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki
Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Africa ya
kusini.

Waziri
mkuu Mizengo Pinda akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa
kanisa la Anglican Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo

Waziri
mkuu Mizengo Pinda na mkewe wakiweka shada ya maua juu ya kaburi la
aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki
Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Africa ya
kusini.

Waziri
mkuu wa zamani Edwald Lowasa akiweka shada ya maua juu ya kaburi la
aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki
Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Africa ya
kusini.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiweka shada la maua kwenye kaburi hilo.
Familia
ya Marehemu Godfrey Mdimi Mhogolo aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la
Anglicani Central Tanganika wakiwa katika eneo la makaburi ambapo
amezikwa nje ya kanisa la Roho Mtakatifu Dodoma. PICHA NA JOHN BANDA
WA PAMOJA BLOG
Post a Comment