Meneja Masoko
na Elimu kwa Umma toka Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi Anjela Mziray akizungumza na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu programu ya upimaji wa Afya kwa
wananchi kwa magonjwa yasiyoambukiza inayoendeshwa na mfuko huo hapa
nchini. Kulia ni Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja na
kushoto ni Afisa habari ,Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Baadhi ya
waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) uliofanyika leo jijini Dar es salaam uliolenga kuelimisha wananchi
kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari,shinikizo la
damu na Saratani.
************************************
Na frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaweka mikakati madhubuti kupambana na magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini.
Hayo
yamesema na Meneja Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya ( NHIF) Bi Anjela Mziray wakati wa mkuatano na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza
Bi Anjela amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
imekuwa ikichukua juhudi za maksudi katika mapambano dhidi ya magonjwa
yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na Saratani za aina
mbalimbali.
Akifafanua
zaidi Bi Anjela amesema programu hiyo imekuja kutokana na ukweli kwamba
magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka na yamekuwa tishio na kusababisha
vifo vya watu wengi nchini na duniani ambapo takwimu za shirika la afya
Duniani za mwaka 2012/2013 watu zaidi ya milioni 35 hufa kwa sababu ya
magonjwa yasiyoambukiza.
Bi
Anjela aliongeza kuwa kati ya waathirika wa magonjwa yasiyoambukiza
milioni 28.1 wanatoka katika nchi zinazoendelea ambapo kwa Tanzania
magonjwa hayo husababisha vifo mara 4 zaidi mijini ambavyo ni sawa
na asilimia 12.8 wakati asilimia 3.1 wapo vijijini.
Akitolea
Mfano Bi Anjela alisema katika zoezi la upimaji lililofanyika Dodoma
Septemba, 2013 jumla ya watu 591 walipimwa kati yao 14 sawa na asilimia
2.3 waligundulika kuwa na kisukari, na 28 sawa na asilimia 5 walikuwa
na shinikizo la damu, wakati watu 128 sawa na asilimia 22 walikuwa na uzito uliokithiri.
Bi
Anjela aliongeza kuwa katika zoezi lililofanyika Mlimani City Jijini
Dar es salaam ocktoba, 2013 watu 450 walipimwa, nusu yao waligundulika
kuwa na uzito uliokithiri na katika zoezi lililofanyika Zanzibar watu
273 walipimwa ambapo kati yao watu 10 sawa na asilimia
3.6 waligundulika kuwa na kisukari, watu 83 sawa na asilimia 30.4
walikuwa na uzito uliokithiri.
Naye Meneja
Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja alitoa wito kwa
wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora ili
kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, msongo wa mawazo na
shinikizo la damu.
Katika
jitihada za Kutoa huduma bora kwa wananchi Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) umebuni mkakati maalum ambao unajulikana kama Afya Bonanza
ambayo ni Kampeni ya kupima afya na kutoa elimu juu ya magonjwa
yasiyoambukiza na inakusudiwa kufanyika mikoa yote hapa nchini ambapo
Zoezi hilo lilizunduliwa rasmi Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam mwezi machi 2014.
Post a Comment