ASKINI
wee! Habari za mjini zinadai kuwa, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel
yuko Dubai akiponda raha huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kuwa jela
jijini Abu Dhabi katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE).Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Sunday.Staa wa filamu Bongo,
Awali,
ilidaiwa kuwa, Aunt aliondoka Bongo kwenda Dubai kuungana na mumewe
katika ndoa, lakini vyanzo vya karibu vikahoji mumewe yupi? Mbona yuko
jela baada ya kudakwa kwa kuishi kinyume cha sheria!
CHANZO CHATIRIRIKA
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, taarifa za mumewe kuwa jela, Aunt
alizichukulia poa kwani baada ya tu ya habari hizo Aunt aliendelea
kujirusha katika kumbi tofauti jijini Dar na hata nje ya Dar kana kwamba
hakuna kitu kilichotokea.
“Aunt hakushtuka chochote taarifa
zilimfikia mapema, lakini hakuchukua hatua yoyote hata kule kuonesha
kwamba amehudhunika,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kama
hamuamini tembeleeni katika kumbi za starehe kila siku tunakula naye
bata kama kawaida, angekuwa mwingine angejaribu hata kuwa karibu na
ndugu wa mume kushirikiana na kujua taarifa za mumewe.”
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Sunday.Aunt Ezekiel akiponda raha.
AUNT ALIPOKEAJE MUMEWE KUFUNGWA?
Kumbukumbu
zilizopo katika makrabasha ya Magazeti Pendwa zinaoonesha kuwa, Aunt
alipoulizwa na mapaparazi wetu kuhusiana na taarifa hizo, alikiri
kuzifahamu lakini akafafanua kuwa mumewe alikamatwa na kuachiwa huru
lakini watu wa karibu wameendelea kupinga.
“Mume wangu amekamatwa
ndiyo lakini si kama watu wanavyosambaza maneno wanayoyajua wao na
kupindisha ukweli, alikamatwa kutokana na suala la kibali cha makazi
kwisha muda wake lakini amesharekebisha, ameachiwa,” alisema Aunt.
HAONEKANI BONGO, DUBAI
Licha
ya Aunt kudai mumewe huyo alikamatwa na kuachiwa, lakini tangu
alipotamka kauli hiyo mwishoni mwa mwaka jana hadi sasa, mwanaume huyo
hajawahi kuonekana hadharani.
“Tangu
alipokamatwa hakutoka tena na ishu yenyewe aliyokamatwa nayo
inasemekana ni mbaya hivyo si rahisi kutoka,” kilisema chanzo hicho bila
kufafanua ni ishu gani.
MAPAPARAZI WETU WAMNASA
Wakati
taarifa hizo zikiendelea kusambaa jijini Dar, mapaparazi wetu waliwahi
kumnasa staa huyo katika viwanja tofauti vya starehe kwenye miji ya
Arusha na Dar es Salaam.
Uchunguzi wa mapaparazi wetu ulionesha
kuwa kabla na baada ya taarifa za mumw kukamatwa kusambaa, Aunt
hakuonesha tofauti, aliendelea kula kunywa na kucheza kama kawaida.
AUNT AENDELEZA BATA
Mapama
wiki hii, Aunt ambaye yupo Dubai aliposti picha katika mtandao wake wa
Instagram na kuonesha jinsi gani anakula raha huko.
Picha
hizo zinamuonesha mrembo huyo akiwa katika bwawa maalumu la kuogelea
(swimming pool) huku akinywa vinywaji tofauti hali ambayo ilileta
tafsiri kwa mashabiki wake kwamba ni kuponda raha huku mumewe akidaiwa
kuwa jela.
“Sasa huyu (Aunt) jamani vipi, badala apambane kujua
hatima ya mumewe yeye yupo bize kula raha za mjini utadhani ana furaha,”
alichangia shabiki
wake mtandaoni.
AWACHEFUA MASHEMEJI
Taarifa
zaidi zimeeleza kuwa mara baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika
mitandao ya kijamii, baadhi ya mashemeji wa Aunt walikuja juu na kudai
wanamshangaa ni vipi haoni hali ilivyo na hawamsikii akizungumzia lolote
kuhusu ndugu yao.
“Mashemeji zake wamekasirika kwelikweli kwani
kuzagaa kwa picha hizo mtandaoni kunaleta tafsiri kwamba Aunt hana
mpango na Demonte,” kilisema chanzo.
WIFI AZUNGUMZA
Katika
kusaka data zaidi za ndugu wa Demonte, paparazi wetu alimtafuta mmoja wa
mashemeji hao wa Aunt ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini
ambapo alisema wamechukizwa na picha hizo na wanajipanga kumpa talaka.
“Huu
si ubinadamu hata kidogo, sasa kwa kuwa ameamua kumwaga mboga sisi
tutamwaga ugali, dawa yake tunamuandalia mipango ya talaka ambapo
tukimpata Demonte kwa njia yoyote na akabariki talaka, tunampa muda
wowote,” alisema shemeji huyo huku akikiri kuwa hata wao hawajui Demonte
yukoje kwa sasa baada ya kupoteza mawasiliano naye.
Source-GPL
Loading...
Post a Comment