SIKU chache baada ya wakazi wa Jiji la Mbeya kupewa tahadhari juu
ya uwepo wa nyoka mkubwa aina ya Chatu katika maeneo ya Rift Valley
pembezoni mwa mto Meta uliopo jijini hapa juhudi za kumsaka zaanza kuzaa
matunda.
Juhudi
za kumsaka Chatu huyo zilianza juzi kwa ushirikiano wa Wataalamu wa
Wanyamapori pamoja na waganga wa jadi ambao walikuwa wakimsaka pembezoni
mwa mtu huo.
Hata
hivyo jitihada za klumsaka Nyoka huyo zilianza kuzaa matunda baada ya
jana asubuhi Waganga hao kufanikiwa kumnasa Chatu mdogo pembezoni mwa
Mto Meta karibu na Hoteli ya Rift Valley.
Kwa
mujibu wa Mganga huyo, Mazoea Hamis(39) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani
alisema siku ya kwanza ya zoezi hilo walifanikiwa kugundua njia
alimokuwa amepita lakini hawakufanikiwa kumpata.
Alisema
jioni yake baada ya kupumzika waliona waweke dawa za kienyeji ambazo
zingiweza kumtoa mafichoni na kusogea karibu ambapo asubuhi waliwahi
kuendelea kumtafuta.
Alisema
baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini kwa
bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo
alipofanikiwa kumkamata.
Kwa
mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi wa
Chunya mkoani hapa, alisema Chatu huyo ni mdogo na juhudi za kuendelea
kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo.
Alisema
mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili
kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na
maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie.
Hata
hivyo taarifa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji zinadai kuwa baada ya
kukamatwa kwa Chatu huyo atahifadhiwa na kutunzwa katika Hifadhi ya
Wanyama ya Ifisi ambako kuna wanyamapori wengine wa maonesho.
NA MBEYA YETU
Post a Comment