Mwigizaji
na muongozaji wa bongomovie Dr. Cheni ambaye alianza kupata umaarufu
kwenye fani ya uigizaji na thamthilia za kundi la Kaole na sasa akiwa
anafanya movie zake, 12 May alizushiwa kifo ikiwa imeunganishwa na ishu
yake ya kulazwa hospitali kutokana na homa ya dengu.Baada ya huo uvumi
kusambaa Elizabeth Michael ”Lulu” aliandika >>> ‘Jamani kuna
mambo ya kuzushiana lakini sio kifo, kuna habari zimezushwa kwamba Dr.
Cheni amefariki, ni habari za uongo jamani…. yuko salama kabisa na juzi
ameruhusiwa kutoka hospital na anaendelea vizuri, tunajua kufa ni wajibu
lakini mpaka Mungu mwenyewe apende….. pole baba angu’
Dr
Cheni na yeye aliandika ‘Jamani kifo kipo na hakuna atakaekwepa ni
lazima tutakufa na hakuna atakaebakia ila si vyema kunizushia, siku
yangu itafika tu na wote mtajua lakini si jambo la busara kunizushia.
Hii ni moja ya picha zilizosambaa kwenye internet zikimuonyesha Dr Cheni akiwa hospitali
on Tuesday, May 13, 2014
Post a Comment