Mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) ambaye
ni mlemavu wa ngozi (albino) mkazi wa kijiji cha
Gasuma kata ya Nkololo wilayani bariadi mkoani Simiyu ameuawa kwa kukatwa
mapanga na watu wasiojulikana ambao wametoweka na viungo vyake.
Kamanda wa polisi mkoani wa Simiyu Charles
Mkumbo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa
marehemu, ambapo wahusika, baada ya kufanya
mauaji hayo walimkata mguu wake wa kushoto, sehemu ya goti, vidole 2 vya mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba
kisha kutoweka navyo.
Chanzo cha tukio hilo
kimetajwa kuwa ni imani za kishirikina na kwamba tayari watu wawili ambao ni waganga
wa kienyeji wanashikiliwa na jeshi la
polisi kwa mahojiano zaidi.
TAARIFA KAMILI KUHUSU TUKIO HILI
ITAKUIJIA.
picha na GPL
chanzo: Malunde1 Blog
Post a Comment