Baadhi ya wanawake wanakunywa maji ya Kondo la Nyuma saa chache baada ya kujifungua
Hugeuka
kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake
wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ?
Kondo
la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu
hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa
tumboni.
Njia za kula Kondo la Nyuma
- Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
- Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
- Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
Baadhi
ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi
kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na
kwamba sio vizuri kuitupa.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Wanasema
kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata
nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo
la nyuma.
'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi
ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa maji yake saa chache tu baada
ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na
wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni
moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo
la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba
kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo
linaposagwa.
Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda
Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni
hiyo ilishitakiwa na wataalamu wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza
kuwa na Bakteria ambayo inaweza kusababisha athari za kiafya kwa
wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo la nyuma.
Charlie
Poulter, kutoka mtaa wa Reading, anaamini kuwa alipokunywa maji ya
kondo la Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie''
"nilikuwa
nimejifungua na nilihisi kuishiwa na nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo
nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo
ingenisaidia kupata nguvu na kupona haraka,'' alisema mama Charlie.
'Kondo la Nyuma ni nini?'
Baadhi ya wanawake huikausha na kuikaanga kama nyama
Hii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na kitovu.
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.
Baada
ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka mwilini mwa mama anaposukuma
mtoto au hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa upasuaji.
Binadamu
kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa
baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama wengine wa kufugwa. Lakini kwa
mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.
Nchini
China baadhi ya madaktari wa kienyeji hutumia sehemu hiyo ya mwili
kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula Kondo la
Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya magharibi.
'Je wanasayansi wanasemaje?'
Hadi leo hakuna utafiti wowote kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.
SOURCE:BBC
SOURCE:BBC
on Monday, May 12, 2014
Post a Comment