Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu
Kiongozi
wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru
wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo
wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika
kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa
wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita
tangu watekwe nyara.
Kanda
hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na
kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana
waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Wakati
huohuo Waziri wa mambo ya ndani nchini Nigeria amesema serikali
haitakubali masharti ya kundi la Boko Haram kwamba kwanza liwaachilie
wapiganaji wake kabla ya wasichana zaidi ya miambili waliotekwa nyara
waachiliwe.
Waziri Abba Moro amsema ni jambo la kipuuzi sana kwa kundi la kigaidi kujaribu kuweka masharti kama hayo.
Mwandishi
wa BBC mjini Maiduguri John Simpson anasema kuwa masharti yaliyotolea
na kundi hilo ni ishara kuwa liko tayari kufikia makubaliano na serikali
Wasichana
watatu kati ya waliooyeshwa na kuongea katika kanda hiyo walikuwa
wanavalia hijabu. Mmoja alisema kuwa amesilimu wakati mwingine akisema
yeye tayari ni Muisilamu.Chanzo BBC
Post a Comment