Wakazi wa Mwananyamala wakiwa eneo la mto Ng'ombe kushuhudia tukio hilo.
MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa
umetupwa eneo la mto Ng'ombe jirani na Rasco, Mwananyamala jijini Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo.
Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Makumbusho, Bi. Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake
kutojihusisha na vitendo viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za
uzazi wa mpango kujikinga na matatizo kama hayo.
"Nina masikitiko makubwa kwa kitendo hiki, ni bora kichanga hiki
kingeletwa serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili. Kama wananchi
mkishindwa kuvumilia bora mtumie uzazi wa mpango," alisema Bi. Husna
huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika!
CHANZO: GPL
Post a Comment