Wanasoka
wa kale na wa sasa nchini Brazil wameanzisha kampeni iitwayo VemIbra
(yaani Njoo Ibra) ili kuhakikisha mshambuliaji nyota wa Sweden Zlatan
Ibrahimovic 32 anakuwepo Brazil kwa ajiri ya kombe la dunia mwezi ujao.Nyota
hao ambao ni Dan Alves,Bebeto,Rai,Denilson na Ronaldo de Lima
wametengeneza video fupi ili kumshawishi Zlatan kuja Brazil kushuhudia
michuano hiyo.
Video
hiyo inaanza kwa kuonyesha magoli ambayo Zlatan amefunga akiwa na klabu
yake ya PSG msimu huu kisha kufuatiwa na goli la Christian Ronaldo
lililofuta ndoto ya mswedeni huyo kuwemo katika michuano ya mwaka huu ya
kombe hilo kubwa na maarufu zaidi duniani.
Baada ya goli hilo kukafuatiwa na nukuu ya Zlatan kufuatia kauli aliyoitoa isemayo
"Kombe la dunia bila mimi hainogi kutazama" Kauli hii ilikuja baada ya Sweden kufungwa na Ureno katika mchezo wa mtoano wa kusaka tiketi ya kombe la dunia.
Baada ya nukuu hiyo unafuata wimbo maalum toka kwa mlinzi Dan Alves akimsihi Zlatan kuja Brazil.
Wimbo huo unafuatiwa na ujumbe toka kwa nyota watajwa hapo juu
(Rai,Ronaldo,Bebeto na Denilson) Baada ya Zlatan kuona video hiyo
akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter
"Brazil!!Itanibidi kupangua ratiba ya likizo yangu" Tusubiri tuone kama kampeni hii itafabikiwa
Post a Comment