Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik amekanusha tuhuma
zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (si HabariLeo) kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Temeke Sophia Mjema ametishiwa maisha baada ya kuvunja
danguro la Temeke.
Akizungumza
ofisini kwake jana, Mkuu huyo wa Mkoa alisema gazeti hilo liliandika
habari hiyo ambayo si ya kweli na kuongeza kuwa ina lengo la kudidimiza
operesheni hiyo.
“Naomba
niwatoe hofu habari hizo si za kweli na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema
ametueleza kuwa si kweli na hivyo tunaamini mwandishi wa habari hiyo
hana lengo zuri,” alisema Sadik.
Aliongeza kuwa danguro hilo lilikuwa ni kichaka cha wanawake wadogo wanaojihusisha na ngono, wavuta bangi na dawa za kulevya.
“Kwa
kweli kama kuna madanguro mengine tunaomba yafichuliwe ili wanaofanya
biashara hizo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria haraka na tunaahidi
kuwa operesheni hii itakuwa endelevu,” alisema.
Aidha
alitoa rai kwa wananchi ambao katika mitaa wanayoishi kuna madanguro
watoe taarifa hizo haraka kwa vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe
mara moja.
Post a Comment