![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sbCQOxnlB5uqbuC6c53LPLf4bx7C1JUN--iP3mfjS-UYt1BD7xni7x3p8D4EyE6DeeUV1UeQQuuyuhqlmyyZDfvsOf2pZsIbOPm-ThwJxDg84bfWPVCNKm-Xz6W_DGFR5OkIKfMvbMvqF_FIvpGrJyvhOycpLBaKbf768hUNkSSWDAom0a0Rz-D7R2H_8VWC2wPAKZh2FErXs3o8x9iEcQ25buujwc5jAg9zmvjVJjn2yQefNBeXk=s0-d) |
Msanii
wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo
Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana
kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali
yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya
na baadae kufariki dunia.
|
Kifo
cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii
mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki
kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili baada ya taarifa za msiba wa msanii mwenzao, Rachel Haule
'Recho' mapema leo.
Mume wa marehemu Recho, George Saguda,akiwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha mkewe. Picha kwa hisani ya GPL
Post a Comment