Katika tukio la kushangaza, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Anord Michael mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya vurugu kubwa nyumbani kwao, akidaiwa kutaka kumuua baba yake mzazi kwa sababu ambazo hazikueleweka sawasawa.
Huku
majirani na watu wengine wakishangazwa na kitendo hicho, Anord
alimfungia ndani baba yake mzazi na kuanza kumshambulia kwa silaha
mbalimbali kabla ya kuchukua panga kwa lengo la kutaka kummaliza kabisa.
Mzee
Michael, kuona kijana wake amepania kummaliza, alipiga mayowe ya kuomba
msaada, kitu ambacho kilifanikiwa kwani mara moja wasamaria wema
walijitokeza na kumuokoa kwa kumhifadhi katika chumba kingine ndani ya
nyumba hiyo.
Pamoja
na hivyo, kijana huyo ambaye bado watu wana mashaka na utimamu wa akili
yake, aliendelea kufanya fujo huku akivunja mlango wa chumba
alichohifadhiwa baba yake ili aweze kumtoa roho, huku pia akitishia
kumuua mtu yeyote ambaye angejaribu kumsogelea.
Akiwa
katika hatua za mwisho kuvunja mlango huo huku baba yake naye akianza
kusali sala ya mwisho kabla ya mauti kumfika, ghafla askari wenye silaha
waliwasili eneo hilo na kuanza kumdhibiti kijana huyo.Hata
hivyo, zoezi la kumdhibiti kijana huyo halikuwa rahisi, kwani bado
alisababisha timbwili kubwa kabla ya maafande hao kutumia ujuzi wa
kikazi bila kutumia risasi na kumweka chini ya ulinzi.
Katika
hali ya kushangaza, baada ya askari polisi kumuuliza sababu iliyomfanya
afikie uamuzi wa kumuua baba yake mzazi, Anord alidai mzee huyo ndiye
chanzo cha yeye kuharibikiwa kimaisha.
Baadaye maafande hao walimzoa kijana huyo na baba yake kuelekea Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama kwa mahojiano zaidi.
Post a Comment