Mahakama
ya mwanzo ya Old Shinyanga imemhukumu Pendo Joachim (33) mkazi wa Old
Shinyanga kifungo cha miezi 12 na kulipa faini ya shilingi milioni moja
kwa kusingizia mtoto kwa mwanaume mwingine ili apate pesa za matumizi.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo Christina Chovenye amesema mahakama hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi imemhukumu Pendo utumikia kifungo hicho cha nje ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Chovenye amesema mahakama hiyo imemtia hatiani Pendo kwa kosa la udanganyifu kwa Deus Njile ambaye amekuwa akimuhudumia mtoto huyo aitwaye Edward Deus kwa muda wa miaka 3 bila kujua kuwa sio mtoto wake.
Taarifa kutoka kwa Deus Njile zimesema kuwa alibaini kuwa mtoto huyo sio wake baada ya kuona kadi mbili za kliniki zenye majina tofauti ya baba ndipo alipoamua kwenda kwenye uongozi wa kijiji ili kupata suluhu.
Njile ameongeza kuwa baada ya kwenda kwenye uongozi wa kijiji, Pendo alikiri kuwa mtoto huyo ni wa mwanaume mwingine.

Post a Comment