Rais
awamu ya tatu Benjamen Mkapa (katikati) mkuu mkoa Singida Dk. Parseko
Kone (kushoto) na mwakilishi wizara ya afya na ustawi wa jamii Dk.
Catherine Joachim, akizindua nyumba ya watumishi wa afya vijijini, kati
ya 30 zilizogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.9 kupitia mfuko wa ‘Mkapa
Foundation’ kwa wilaya za Mkalama, Iramba, Singida, Ikungi na Manyoni
Mkoani Singida.
Mkuu
Mkoa Singida Dk. Parseko Kone akimkabidhi hati ya nyumba mganga mkuu wa
Wilaya Iramba Dk Japhet Simeo mara baada ya rais mstaafu Benjamen Mkapa
kukabidhi nyumba za kisasa 30 kwa watumishi wa afya vijijini
zilizojengwa na taasisi ya Mkapa foundation, kwa wilaya za Manyoni,
Ikungi Mkalama, Singida na Iramba, makabidhiano yaliyofanyika kijiji cha
Senenemfuru halmashauri ya wilaya Singida.
Rais
awamu ya tatu, Benjamen Mkapa akikabidhiwa kibuyu na akina mama wa
kijiji cha Senenemfuru Singida vijijini, kikiwa na maana ya upendo,
kwenye hafla ya kukabidhi nyumba, kati ya 30 zilizojengwa na Mkapa
foundation kwa halmashauri tano za mkoa wa Singida.
Mwonekano
wa nyumba iliyojengwa na taasisi ya Benjamen Mkapa katika kijiji cha
Senenemfuru halmashauri ya wilaya Singida, kati ya 30 zilizojengwa
katika wilaya tano mkoani Singida kwa ajili ya watumishi wa afya
vijijini kwa gharama ya Sh.1,945,187,143.Picha na ELISANTE JOHN-Singida.
Na Elisante John, Singida
RAIS
mstaafu awamu ya tatu Benjamen W. Mkapa kupitia taasisi yake ‘Benjamen
William Mkapa HIV/AIDS’ (BMAF), amekabidhi nyumba 30 zilizojengwa kwenye
zahanati 13 na vituo vya afya viwili kwa zaidi ya Sh. Bilioni 1. 9,
katika halmashauri tano za Wilaya Mkoani Singida.
Akikabidhi
sehemu ya nyumba hizo jana kwenye hafla iliyofanyika kijiji cha
Senenemfuru Singida vijijini, mzee Mkapa alishukuru wafadhili
waliowezesha kazi hiyo, ukiwemo mfuko wa dunia wa kupambana na Ukimwi,
kifua kikuu na malaria (Global fund), kwa kuonyesha imani na serikali ya
Tanzania.
Nyumba
hizo zimejengwa katika zahanati ya Misughaa na Mangonyi (Ikungi),
Mkenge, Mpambaa na Senenemfuru (Singida), Ulemo Uwanza na kituo cha afya
Ndago (Iramba), Kinyambuli na Dominiki (Mkalama), pia kituo cha afya
Itigi, Idodyandole, Heka, Mpola na Chibumagwa (Manyoni).
Post a Comment