SHULE ya Sekondari ya Pugu, iliyopo maeneo ya Pugu jijini Dar es
Salaam, ambayo inasifa kubwa nchini kwa kuwa iliwahi kufundishwa na Baba
wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere, imevamiwa na wadudu aina ya
kunguni ambao wanadaiwa kuwasumbua wanafunzi wa bweni wa shule hiyo.
Akizungumza na waandishi wetu, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,
Agustino Angelo, alisema tatizo hilo limekuwepo muda mrefu na
wamejitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa kwa kufanya upuliziaji
(fummigation) mara mbili huku naye Mstahiki Meya wa Ilala Jerry Slaa,
akiahidi kulimaliza kabisa tatizo hilo katika siku za hivi karibuni.
Waandishi wetu walizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo,
ambao walikiri kusumbuliwa na tatizo hilo ambalo wanadai kuwa
linawakosesha amani na kuwataka viongozi wa serikali wajitokeze
kutokomeza tatizo hilo ili waendelee na masomo yao vizuri.
Mbali na hayo, waandishi wetu pia walishuhudia majengo chakavu ya
shule hiyo, mazingira ambayo si rafiki na heshima ya shule hiyo yenye
historia kubwa nchini.
(Picha: Chande Abdallah na Denis Mtima / GPL)
Post a Comment