Naibu
Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) akila kiapo
cha utii na utumishi mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto).
===== ====== =====
Na Saidi Mkabakuli.
Serikali
imeweka wazi mkakati wa kuainisha fursa za kipaumbele zitakazoiwezesha
kuivusha nchi kikanda na kimataifa kwa kusimamia na kufuatilia
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama inavyobainishwa na Mpango wa
Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Miaka Mitano (FYDP I) unaosimamiwa na
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mkakati
huo umewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya
Kiuchumi Bw. Paul Sangawe mara baada ya kula kiapo cha kuitumika nafasi
hiyo. Bw. Sangawe
amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuongeza mauzo ya bidhaa
na huduma pamoja na kufaidika na misaada kutoka nchi marafiki na
mashirika ya kimataifa.
“Kwa
mujibu wa Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa Mwaka 2012/13 thamani ya mauzo
ya bidhaa na huduma nje ilikuwa dola za Kimarekani 6,796.3 milioni mwaka
2011, ikilinganishwa na dola 5,805.0 milioni mwaka 2010 sawa na
ongezeko la asilimia 17.1. hivyo mkakati wetu ni kuongeza hali hii,”
alisema Bw. Sangawe.
Kwa
mujibu wa Mpango huo thamani ya bidhaa za kukuza mitaji zilizoagizwa
toka nje iliongezeka hadi dola za Kimarekani 3,560.5 milioni kutoka dola
2,715.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 31.1. Ongezeko
hili lilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uagizaji wa mitambo hasa ile
ya viwandani.
Aidha,
thamani ya uagizaji wa bidhaa za kati iliongezeka hadi dola za
Kimarekani 4,139.0 milioni mwaka 2011, kutoka dola 2,741.2 milioni mwaka
2010, sawa na ongezeko la asilimia 51.0. Uagizaji wa mafuta kwa wingi
ulitokana na matatizo yaliyojitokeza ya kutozalishwa kwa kiasi
kinachohitajika cha umeme unaotokana na maji, hivyo kupelekea mitambo
mingi ya mashine kuendeshwa kwa kutumia umeme unaozalishwa na mafuta.
Vilevile,
thamani ya mafuta yaliyoagizwa katika mwaka 2011 ilikuwa dola milioni
3,228.7 ikilinganishwa na dola milioni 2,024.2 mwaka 2010. Uagizaji wa
bidhaa za matumizi ya kawaida uliongezeka hadi dola 2,128.0 milioni
kutoka dola 1,709.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia
24.5.
Bw.
Sangawe ameongeza kuwa Serikali inajikita katika kutambua masoko kwa
bidhaa za Tanzania na vyanzo vipya vya uwekezaji katika uchumi wa Dunia
na Kikanda ili kuwezesha sekta binafsi kuchangia kufanikisha utekelezaji
wa miradi hiyo ya maendeleo ili kuwezesha nchi kuchanmkia fursa za
masoko ya kimataifa ikiwemo AGOA na nchi za jumuiya za Ulaya.
“Kipaumbele
itakuwa ni kutumia rasilimali chache kuchochea uwekezaji wa sekta
binafsi pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji
ili kuvutia uwekezaji katika maeneo ya kipaumbele na ya matokeo
makubwa,” aliongeza Bw. Sangawe.
Serikali
imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na
mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la
Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
Post a Comment