WABUNGE
wameendelea kuchangia hotuba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kutenga
Taifa Dk. Hussein Mwinyi aliyoitoa jana. Vifuatavyo ni baadhi ya
vidokezo vilivyochangiwa na waheshimiwa wabunge wa Bunge la 10 Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, mkutano wake wa 15 kwenye kikao chake cha Saba.
Wataalamu tunao, tumewatelekeza- Anna Abdalah
MBUNGE wa Viti Maalum, Anna Abdalah amesema nchi imewatelekeza wataalamu mbalimbali waliopo jeshini, ambao wanakaa kambini wakiwa hawana kazi ya kufanya. Alisema baadhi ya zana za kivita zinaweza kutengenezwa katika sehemu kama Nyumbu, lakini kutokana na ukosefu wa fedha za kuendeshea kitengo hicho, matokeo yake askari hao wameendelea kukaa kambini bila kazi na hivyo kutotumika kwa vipaji vyao.

Aidha,
mbunge huyo mkongwe alisema alama nyingi za mipakani ambazo ziliwekwa
na Jeshi zimeondolewa na hivyo kutojulikana wapi ni wapi, hasa katika
mipaka ya nchi jirani.
Wanaofariki nje hulipwa na nani?
Wabunge wamehoji juu ya askari wanaotumika kulinda amani katika baadhi ya nchi duniani, kwamba wanalipwa na nani kati ya serikali au Umoja wa Mataifa, kwani wanapokuwa huko, hutumika chini ya kofia ya UN.

Wametaka
pia kujua idadi ya askari waliofariki dunia wakiwa katika utumishi huo
nje ya nchi na kutaka kufahamishwa jinsi familia zao zinavyolipwa fidia.
Mbona fedha za Jeshi zinacheleweshwa?
WAbunge pia wamezungumzia suala la Wizara ya Fedha kushindwa kupeleka fedha za Wizara ya Ulinzi kwa wakati kwa visingizio kwamba fedha hakuna, wakati inajulikana kuwa fedha zipo.
WAbunge pia wamezungumzia suala la Wizara ya Fedha kushindwa kupeleka fedha za Wizara ya Ulinzi kwa wakati kwa visingizio kwamba fedha hakuna, wakati inajulikana kuwa fedha zipo.
Walisema
ni jambo la hatari kwa nchi iwapo askari ambao hufanya kazi usiku na
mchana kwa ajili ya kulilinda taifa lao, litachoka kusubiri fedha,
wakitolea mfano kuwa mwaka jana walipokea kiasi cha asilimia 20 tu ya
fedha zao za bajeti.
Masilahi ya wastaafu yaliliwa
Kapteni Mstaafu wa Jeshi, John Chiligati amesema ulipwaji wa mafao ya askari wastaafu wa Tanzania hauko vizuri na kupendekeza nchi ijifunze kutoka India, kwani huko, licha ya kulipwa vizuri, lakini pia huwezeshwa kwa namna mbalimbali ili wasipate taabu katika maisha yao.

Alisema
kwa vile askari hustaafu kulingana na vyeo vyao, wale wenye ujuzi wa
aina mbalimbali, hutafutiwa kazi mbadala uraiani au kukopeshwa pesa na
vyombo vya fedha ili waweze kujiajiri kwa kutumia taaluma zao uraiani.
Maonyesho ya Jeshi Dar yawagawa
Katika michango hiyo ya wabunge, baadhi yao walitofautiana kuhusiana na maonyesho yaliyofanywa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam April 26 mwaka huu.

Mmoja
wa wachangiaji hao alishangaa ni kwa namna gani Jeshi hilo liliweza
kuanika silaha zake hadharani, kwani kwa kufanya hivyo, ni rahisi kwa
adui kujua namna ya kukabiliana naye. Alikifananisha kitendo hicho na
mtu kuonyesha kila kitu chake hadharani, ikiwemo nguo yake ya ndani.
Hata
hivyo, wachangiaji wengine walisema maonyesho hayo ni jambo la kawaida
na kwamba baadhi ya nchi kubwa nazo hufanya namna hiyo, wakizitaja kama
China, India na Marekani.
Wahindi wapigwe marufuku Jeshini
Mbunge mmoja alimtaka Waziri Mwinyi kuangalia uwezekano wa kuwaondoa wafanyabiashara wa Kihindi katika maduka makubwa yaliyo ndani ya kambi za kijeshi (Supermarkets) na kutaka kazi hiyo kupewa wazawa.

Huku
akisisitiza kuwa hakuwa mbaguzi wa rangi, alisema kazi za kuendesha
maduka hayo, tena ndani ya kambi za jeshi, inapaswa kufanywa na
watanzania wazawa, hasa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
Aidha,
mbunge mwingine alishangaa na kuhoji kwa nini bei za bidhaa katika
maduka ya jeshi zimekuwa sawa na maduka ya uraiani wakati kule jeshini
kuna msamaha maalum wa kodi kiasi cha asilimia 18.
Hee, Tanzania ya 20 nguvu za kijeshi Afrika
Katika hali isiyotarajiwa, mbunge mmoja alisema licha ya mbwembwe nyingi zilizoonyeshwa na Jeshi la Wananchi siku ya Muungano jijini Dar es Salaam, Tanzania ni ya 20 kwa majeshi yenye nguvu barani Afrika, kwa mujibu wa mitandao inayozungumzia nguvu za majeshi duniani (hakutaja mtandao huo).

katika mataifa yote duniani, Tanzania inashika nafasi ya 102 kwa nguvu
za kijeshi, huku akiponda kuwa nchi yetu inazidiwa hata na nchi za
Uganda na Rwanda ambazo zipo juu kimsimamo, kwa sababu ya kile
alichosema serikali kushindwa kuipa wizara husika fedha za kutosha
kuweza kujitosheleza.
Wanaopitia JKT, JKU janga la kitaifa
Baadhi ya wabunge pia walisema kuwaacha bila kuwapa ajira vijana wanaomaliza mafunzo ya kijeshi katika majeshi ya JKT na JKU ni janga la kitaifa kwa sababu wanapofika uraiani na kukutana na ugumu wa maisha, wanaweza kufanya lolote ili kukabiliana na ugumu huo.

wakiwa wanafahamu kutumia aina mbalimbali za silaha, ni rahisi kwao
kushawishika kwenda kushiriki matukio ya uhalifu, endapo atajitokeza mtu
na kuwaeleza juu ya uwezekano wa kupata kiasi kikubwa cha fedha.
Kwa
ajili hiyo, waliitaka wizara kuwapa kipaumbele vijana hao wanaomaliza
mafunzo katika ajira, ikiwa ni njia ya kusaidia kuokoa vijana ili
wasijihusishe na vitendo vya kihalifu.
Kupima Ukimwi iwe lazima JWTZ
Mbunge mwingine alisema kwa kuwa vijana wa JWTZ wana jukumu kubwa la kuhakikisha mipaka ya nchi yetu inakuwa salama muda wote, wakati sasa umefika kwa kila anayetaka kuajiriwa, lazima apimwe afya yake ili kujiridhisha.

jambo hili linapaswa kuzingatiwa hasa kwa vile kama hali itaachwa
iendelee hivi hivi, ipo siku taifa linaweza kujikuta likimpeleka mtu
mgonjwa vitani, ambaye anaweza kufariki kabla ya kufika katika uwanja wa
mapambano.
Aidha,
walisema wanajeshi wanapata ugonjwa huo kutokana na kuachwa nyuma kwa
wake au wapenzi wao wakati wanapohama kutoka kambi moja kwenda nyingine,
kitu kinachowafanya wachepuke.
on Tuesday, May 13, 2014
Post a Comment