AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO
Telephone: 0222110585
email:maelezopress@yahoo.com
|
IDARA YA HABARI(MAELEZO)
S.L.P.9142,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
26,MEI, 2014
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DKT.MUKANGARA AMLILIA MAXIMILIAN
Waziri
wa Habari Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za
rambirambi waandishi wa habari kufuatia kifo cha Mpiga picha wa kituo
cha television cha Mlimani, Ndugu Maximilian John kilichotokea alfajiri
ya kuamkia Jumamosi wiki iliyopita.
Dkt.
Mukangara amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha
Bwana Maximilian kilichotokana na maradhi ya Moyo, Sukari na Shinikizo
la damu na ameongeza kuwa kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia
ya habari hapa nchini.
Amesema Bw.
Maximilian atakumbukwa kwa uchapakazi na uhodori wake wa kazi zake
uliokuwa unazingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari, jambo
lililomfanya awe na marafiki wengi wa tasnia hiyo.
“Nakutumia
salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu mkubwa kwa watumishi wote wa
Mlimani TV, tasnia ya habari na familia yake kwa ujumla, amesema Dkt.
Mukangara.
Ameongeza
kuwa Bw. Maximilia atakumbukwa daima na waandishi wa habari na wadau
wengine kwa ucheshi wake,ushirikiano na wenzake wakati wa kutekeleza
majukumu ya kitaalum na ujenzi wa Taifa kupitia Sekta ya habari.
“Ninaungana
na waandishi wa habari na wadau wengine katika kumwomba Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu. Amen,” amesema
Dkt.Mukangara.
Imetolewa na;
IDARA YA HABARI, VIJANA , UTAMADUNI NA MICHEZO
26 Mei, 2014



Post a Comment