Serikali imepandisha maradufu ada kwa wanafunzi wanaosomea ualimu kwenye vyuo vya ualimu nchini kuanzia muhula ujao wa masomo.
Ada
hizo kwa wale wa ngazi za cheti na stashahada ambazo zimeongezwa kwa
karibu mara mbili au zaidi ya zile zilizokuwa zikilipwa awali. Uamuzi
huo ambao huenda ukawaathiri zaidi wanafunzi ambao waliona ualimu kama
kimbilio, unaelezwa na baadhi ya wadau wakiwamo walimu, wanafunzi na
hata wakufunzi wa baadhi ya vyuo nchini kuwa ni wa ghafla.
Kwa
mujibu wa baadhi ya wakufunzi, uamuzi huo umetolewa kupitia waraka wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na unatarajiwa kuanza kutekelezwa
muhula wa pili wa masomo utakaoanza Julai 2, mwaka huu.
Kabla
ya kupandishwa kwa ada hizo, wanafunzi wanaosomea ualimu kwa ngazi ya
cheti walikuwa wakilipa Sh200,000, lakini sasa watalazimika kulipa
Sh300,000, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50.
Kwa
wale wanaochukua stashahada watalazimika kulipa Sh400,000 kwa masomo ya
Sanaa na Sh600,000 kwa masomo ya Sayansi kutoka Sh200, 000 za awali.
Post a Comment