Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

COUTINHO AWASILI NA KUSEMA AMEKUJA KUISAIDIA YANGA SC

Afisa Haari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa pamoja na mshambuliaji mpya Andrey Coutinho mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerer leo
**********
Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC  Andrey Marcel Ferreira Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini Brazil tayari kabisa kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani katika msimu wa 2014/2015.
Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja Tanzania imemkchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo ndipo anapoishi>
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege  wa JK Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa habari walijitokeza kumlaki.
Akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege Coutinho amesema anajisikia furaha kuwa Tanzania, nchi ambayo watu wake wanapenda mpira na kikubwa amekuja kuisaidia Yanga kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali mbali itayakayowakabili.
Kuhusu changamoto za ugeni katika Bara la Afrika, Coutinho alisema soka kwake ni kazi, ana uzoefu baada ya kucheza pia Barani Asia hivyo hana wasiwasi, na kwa kuwa na walimu aliwazoea anaamini kwa pamoja atafanya vizuri.
Msafara wa kutoka Uwanja wa ndege ulielekea makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani ambapo Coutinho aliwasilimia wapenzi, washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha aliongea na katibu mkuu Bw Beno Njovu kabla ya kwenda kupumzika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top