Hii
ni neema nyingine kwa Diamond Platnumz, baada tu ya kuwa verifie kwenye
mtandao wa twiter, hatimaye sasa kuwa Verified kwenye mtandao wa
kijamii wa Facebook,
hii
inamaanisha kuwa kampuni ya Facebook hivi sasa inamtambua Diamond
Platnumz kuwa kama msanii maarufu wa kimataifa, nafasi hii wanatokea
kupata wasanii wachache sana na watu maarufu ambao wanapata bahati ya
kujulikana na makampuni makubwa kama haya. Mwanamitindo wakimataifa
Flaviana Matata ni mmoja wa watu maarufu watokao nchin Tanzania
wanaotambuika na kampuni hiyo, na ni moja ya watu maarufu ambao account
yao ipo Verified kama hii ya Diamond Platnumz. Huu ni mwaka mzuri sana
kwa Diamond Platnumz kwa matukio yanayoendelea kumtokea, na kuzidi kumpa
jina kubwa ulimwenguni kupitia muziki wake huu wa Style yake ya kipekee
iliyopewa jina la AfroPop.
Post a Comment