Kufuatia Mahakama ya Ilala jijini Dar kumuachia kwa dhamaa Emmanuel Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji wa nyimbo za Injili maarufu nchini Flora Mbasha anayekabiliwa na tuhuma nzito za kumbaka mdogo wa mkewe, inaelezwa kuwa siku moja tu aliyokaa mahabusu ilimfanya kubadilika muonekano kutokana na kudhoofika.....
Emmanuel
Mbasha ambaye alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza juni
17 mwaka huu na kukosa dhamana kutokana na kushindwa kutimiza
mashariti, alilazimika kutupwa mahabusu katika gereza la Keko,
kabla ya juni 19 kupandishwa tena kizimbani ambapo aliachiwa
kwa dhamana baada ya kutimiza masharti hayo....
Baadhi
ya watu ambao walimshuhudia Mbasha katika viunga vya mahakama
hiyo walioneklana kulengwa na machozi huku wengine wakitamka
kwamba wanamuachia Mungu.....
Mume
huyo wa Flora aliwasikitisha zaidi watu kutokana na kuwa na
mawazo mengi huku miguuni akiwa amevaa malapa ambayo thamani
yake haizidi sh. 2000 wakati katika hali ya kawaida huwa
anavaa mavazi ya bei mbaya na kujiweka msafi muda wote.....
"Maskini
Imma amevaa ndala na amekonda.Hakika yupo katika kipindi
kigumu sana. Jela mtu hukonda siku moja tu.Jela siyo kuzuri
hata hata kidogo," alisema raia mmoja nje ya mahakama hiyo.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Wilberforce Luhwago aliahirisha kesi hiyo hadi July 17 mwaka huu itakapo tajwa tena.....
Baada
ya kuachiwa, Mbasha alitoka nje ya mahakama hiyo kwa kasi na
kuingia kwenye gari kisha kutoweka eneo hilo....
Akizungumza
na mwanahabari wetu, mmoja kati ya ndugu wa Mbasha ambaye
hakupenda jina lake litajwe alisema kuwa mume wa mwanamuziki
huyo aliwaambia hana hamu na jela,
"Mbasha
alisema kuwa jela hakufai kabisa na alisisitiza kuwa asaidiwe
kutoka kwa dhamana. Alisema siku moja aliyoishi mahabusu ni
kama mwaka mzima," alisema ndugu huyo.
Aidha
ndugu huyo alisema kwamba kitendo cha Flora kutomtembelea mume
wake ni cha kinyama na hakuna aliyekitarajia.
"Hakwenda
kumuona mume wake.Kwa kweli jambo hili limetushangaza sana na
kutuumiza sana, sijui mwisho wake utakuwa vipi lakini tunaamini
yatakwisha, kwa uzuri au ubaya," alisema.
Baadhi ya mahabusu ambao walikuwa selo moja na Mbasha katika gereza la Keko wamesema kwamba wamefurahi kuwa na nyota huyo kwani wamekuwa wakimsoma kwenye magazeti tu
Post a Comment