Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FLORA MBASHA NA MUMEWE WADAI WANATAMANI KURUDIANA....!!!

 

Kwa nyakati tofauti jana, kila mmoja wao alimwambia mwandishi wetu kwamba yupo tayari kurudiana na mwenzake, hatua ambayo inaweza kuondoa mgogoro huo ambao umefifisha taswira yao ya kiutumishi.
Akizungumza nyumbani kwake Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Mbasha alisema ameshamsamehe mkewe na kwamba anamsubiri muda wowote arudi nyumbani kusuluhisha mgogoro wao. 'Nawapenda Watanzania wote wazidi kutuombea ili mimi na mke wangu turudiane.' Mbasha alimwambia mwandishi wa gazeti la Mtanzania. 
Kauli hiyo ni sawa na ile aliyoitoa Flora wiki iliyopita pale aliposema: 'Ninawaomba Watanzania waendelee kuniombea ili niweze kushinda majaribu haya, kilichotokea ni sehemu tu ya kupimwa imani yangu'. 
Jana, Flora alirudia kauli hiyo kupitia kwa wakili wake, Addo Mwasongwe ambaye alisema mwimbaji huyo yupo tayari kukutana na mumewe na ndugu ili waondoe tofauti zao. Kwa upande wake Mbasha alisema: 'Mi namwomba Flora ajishushe akubali, aje home (nyumbani) tuyamalize na maisha yaendelee. Yeye ni mke wangu namtaka. Kama ananipenda arudi, tuite wazazi tutatue mgogoro huu.' 
Aliongeza kuwa hakuna binadamu yeyote asiyesamehewa na kwamba kilichotokea katika ndoa yao ni sehemu ya maisha ambayo wengi hupitia. 'Siku zote naamini tunachotakiwa ni kujenga na siyo kubomoa'¦ Flora asing'ang'anie kwa watu arudi hapa'¦ apige hodi'¦ 'mume wangu' nimerudi '¦na mimi nitampokea tuendelee kulea watoto.
'Alisema Mbasha Mbasha anakabiliwa na tuhuma za kumbaka shemejiye wa miaka 17 na kesi yake inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na sasa yupo nje kwa dhamana. 
 *Source:Mtanzania*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top