Kuna kila dalili kwamba mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili
nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha wanatamani kurudiana,
baada ya kuwapo mgogoro katika uhusiano wao wa ndoa, ulioingia katika
vyombo vya habari yapata mwezi mmoja sasa.
Kwa nyakati tofauti jana, kila mmoja wao
alimwambia mwandishi wetu kwamba yupo tayari kurudiana na mwenzake,
hatua ambayo inaweza kuondoa mgogoro huo ambao umefifisha taswira yao ya
kiutumishi.
Akizungumza nyumbani kwake Tabata Kimanga, Dar es
Salaam, Mbasha alisema ameshamsamehe mkewe na kwamba anamsubiri muda
wowote arudi nyumbani kusuluhisha mgogoro wao.
“Nawapenda Watanzania wote wazidi kutuombea ili mimi na mke wangu turudiane.”
Kauli hiyo ni sawa na ile aliyoitoa Flora wiki
iliyopita pale aliposema: “Ninawaomba Watanzania waendelee kuniombea ili
niweze kushinda majaribu haya, kilichotokea ni sehemu tu ya kupimwa
imani yangu”.
Jana, Flora alirudia kauli hiyo kupitia kwa wakili
wake, Addo Mwasongwe ambaye alisema mwimbaji huyo yupo tayari kukutana
na mumewe na ndugu ili waondoe tofauti zao.
Maelezo ya Mbasha
Kwa upande wake Mbasha alisema: “Mi namwomba Flora
ajishushe akubali, aje home (nyumbani) tuyamalize na maisha yaendelee.
Yeye ni mke wangu namtaka. Kama ananipenda arudi, tuite wazazi tutatue
mgogoro huu.”
Baba Mzazi Wa Emmanuel Mbasha.
Aliongeza kuwa hakuna binadamu yeyote asiyesamehewa na kwamba kilichotokea katika ndoa yao ni sehemu ya maisha ambayo wengi hupitia.
Aliongeza kuwa hakuna binadamu yeyote asiyesamehewa na kwamba kilichotokea katika ndoa yao ni sehemu ya maisha ambayo wengi hupitia.
“Siku zote naamini tunachotakiwa ni kujenga na
siyo kubomoa… Flora asing’ang’anie kwa watu arudi hapa… apige hodi…
‘mume wangu’ nimerudi …na mimi nitampokea tuendelee kulea watoto.”
Mbasha anakabiliwa na tuhuma za kumbaka shemejiye
wa miaka 17 na kesi yake inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala
na sasa yupo nje kwa dhamana.
Kauli ya Flora
Wakili Mwasongwe alisema: “Flora amesema ameshayatoa rohoni
masuala yote ya mgogoro na mumewe na leo (jana) aliniambia anataka
kusuluhishwa hata kesho (leo) lakini nimeshindwa kuwakutanisha kwa
sababu nipo ‘busy’.
“Ila nilimwambia Ijumaa hii nitafanya hivyo kwa kuwakutanisha yeye (Flora), Mbasha na wazazi wake ili kumaliza tofauti hizo.”
Wakili huyo alisema awali alikutana na wazazi wa
Mbasha lakini hawakufikia mwafaka, lakini kwa sasa anaamini mambo
yatakwenda vizuri.
Post a Comment