Mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akipelekwa mahabusu ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar.
...Askari Magereza akifunga mlango wa mahabusu.
...Emmanuel Mbasha akielekea kizimbani.
MUME
wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) anayekabiliwa na kesi ya ubakaji
amepewa dhamana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar baada ya
kutimiza masharti.
Mbasha
amefikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Keko alikopelekwa Juni
17 mwaka huu akikabiliwa na kesi ya kumbaka shemeji yake.
Mbasha
baada ya kutolewa kwenye mahabusu ndogo ya mahakamani hapo alionekana
mnyonge na aliyechoka hali iliyosababisha simanzi kwa ndugu na jamaa
zake waliokusanyika mahakamani hapo.
Baada
ya kesi hiyo kutajwa, rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la
George Mushi na baba wa mtuhumiwa huyo, Mwahimu Juma walifanikiwa
kutimiza masharti ya dhamana.
GPL
GPL
Post a Comment