Utabakia Stevie? Hodgson ana matumaini ya kutompoteza Gerrard
ROY Hodgson atajaribu kumshawishi Steven Gerrard ili aendelee kucheza soka la kimataifa mpaka 2016.
Nyota
huyo amebaki njia panda juu ya hatima ya soka lake la kimataifa
kutokana na matokeo mabaya ya kombe la dunia, lakini bado anahitajika na
klabu yake ya Liverpool itakayoshiriki michuano ya UEFA msimu ujao.
Japokuwa
Gerrard, 34, ameshindwa kutamba kombe la dunia, thamani yake na uzoefu
wake unahitaji katika kikosi cha England na Hodgson anatamani kuona
anaendelea kucheza licha ya vijana wengu kuchipukia kwasasa.
Frank
Lampard anajiandaa kustaafu soka la kimataifa, kwahiyo Gerrard atabaki
mchezaji pekee mkongwe na England haitaki kumpoteza kwasababu
anawaunganisha vijana katika kikosi hicho.
Hata hivyo, Gerrard ataifikiria klabu yake ambayo ina mechi ngumu msimu ujao baada ya kufuzu UEFA.
Gerrard
amesema atafanya maamuzi baada ya kuzungumza na marafiki, familia na
kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers baada ya kombe la dunia.
Mawazo
Rodgers yatakuwa muhimu zaidi na inaonekana kocha wa Liverpool na
madaktari wa timu watapenda kumpa mapumziko Gerrard baada ya kombe la
dunia.
Hata
kama mwenyekiti wa FA , Greg Dyke amemhakikishia kazi Hodgson mpaka
2016 licha ya kuchemsha kombe la dunia, mechi ya mwisho dhidi ya Costa
Rica itakuwa muhimu sana na kama England itapoteza, kocha huyo atakuwa
katika mazingira mabaya.
Gerrard akiwatazama wachezaji wa Uruguay walipokuwa wanashangilia bao la pili na la ushindi.
Post a Comment