Pamoja na
kukutana kwenye nyimbo za Kigoma AllStars, kwenye wimbo wa Dully Sykes
‘Utamu’ na kwenye ngoma ya Victoria Kimani ‘Prokoto’, Ommy Dimpoz na
Diamond Platnumz hawajawahi kuachia wimbo rasmi wa pamoja.
Hivi
karibuni Diamond alimpa shavu hitmaker wa ‘Ndagushima’ Ommy kwenye video
ya wimbo aliomshirikisha Iyanya iliyofanyika jijini London, Uingereza
na kuenea tetesi kuwa wawili hao wamepanga kufanya collabo kubwa ya
pamoja itakayokuwa na video kali.
“Watu kwanza najua wanasubiria kwa hamu sana lakini trust me
nakuambia siku utakayosikia moto umewaka basi itakuwa ni balaa na
unaelewa kwamba wamanyema kwanza hawakosei. Sijui itakuwaje, lakini ni
balaa. Halafu projects zipo nyingi tu lakini watu wasubirie tu waone
itakuwaje lakini nakuambia ukweli itakuwa hatari sana,” alisema Ommy
Post a Comment