MWILI wa Idd
Shamba aliyefariki dunia kwa ajali ya barabaraba katika Kijiji cha
Engaruka wilayani hapa, imekaa barabarani kwa zaidi ya saa 21 ikisubiri
polisi na daktari kufika eneo la tukio kwa ajli ya kupima ajali hiyo na
kuufanyia uchunguzi mwili huo kabla kwenda kuzikwa.Polisi walifika eneo
la tukio majira ya saa saba mchana ikiwa ni saa 18 tangu kutokea kwa
ajali hiyo ambapo baada ya kumaliza kazi ya kukagua na kupima eneo la
ajali, mwili huo ulihamishiwa chini ya mti kuukinga na jua usiharibike
wakati wakisubiri daktari kuja kuufanyia uchunguzi.Tanzania Daima
ilishuhudia wananchi na viongozi wa Kata ya Engaruka wakiulinda mwili
huo wakati akisubiriwa daktari kutoka Mto wa Mbu ambaye naye alifika
eneo la tukio majira ya saa 10 jioni.Ajali hiyo ilitokea Juni 12 mwaka
huu baada ya Shamba kudondoka kutoka kwenye gari la mizigo aina ya
Toyota DCM, lenye namba za usajili T 995 AMB lililokuwa likitokea
mnadani Engaruka kwenda Kijiji cha Selela.
Diwani wa kata hiyo, Pashet Sengerwan
(CCM), alisema kuwa mwili huo ulifanyiwa uchunguzi kwenye eneo la ajali
kisha kuzikwa Juni 13, majira ya saa 11 jioni kwenye makaburi ya
kijijini hapo bila kuwasubiri ndugu zake waliokuwa wakitokea
Singida.Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alisema tayari
wameshamhoji mmiliki wa gari hilo, Sauli Kitomari huku wakiendelea na
juhudi za kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alitoroka mara baada ya
kutokea ajali hiyo.
Alisema
kuchelewa kwa polisi kufika eneo la tukio, kulitokana na kukosekana kwa
kituo cha polisi kwenye eneo la Engaruka ambalo pia lina tatizo la
mawasiliano ya simu.
Kwa upande wake,
Mkuu wa Wilaya ya Moduli, Dowika Kasunga, alisema hali hiyo
ilisababishwa na tatizo la mawasiliano na mamlaka husika kwani katika
Kata ya Engaruka ili upige simu, lazima uende umbali mrefu kutafuta
mawasiliano hayo.
Post a Comment